Kiukweli kwa mtazamo wangu kwa sasa nimeshuhudia akinadada wengi wakifunga ndoa tayari wakiwa ni wajawazito na kutoka na uchunguzi niliofanya ukiwauliza wanaume wanakuambia lazima ujaribu kwanza kama mwanamke anauwezo wa kupata mtoto au la,wengine wanasema inakuwa ni bahati mbaya,au unakuta imetokea binti amepata ujauzito na hivyo kutaka pindi atakapopata mtoto awe ndani ya ndoa, na wanawake waliowengi wanasema inabidi kuangalia kama nitapata mtoto ili kuepusha maneno kwa ndugu wa mume.majibu yalikuwa yanatofautiana lakini mimi nikaona ni kama kutokujiamini kwa mawazo kama hayo . |
Maoni 3 :
Nafikiri inatokea tu au labda wanapenda. Ila hiyo ya kusema eti wanajaribu kwa kweli napingana nayo kwani inaonekana kama hakuna penzi hapo. ETI KUJARIBU mmmhhh!!
wengine bahati mbaya, wengine mr anakupima kwanza no ndoa bila mimba, kina dada nasi tunadhani tukibeba mimba ndo tutaolewa,wengine wana hamu ya mtoto, just sielewi elewi. tuone na wengine.
Gg
mimba kwanzaa ndoa badayee ndo mpango mzima siku hizi
Chapisha Maoni