Alhamisi, Novemba 11, 2010

Mwanamke abakwa na wanaume 6 kisha kuchanwa viwembe sehemu za siri hadi kufa,,,watuhumiwa wanatafutwa...

Wanawake tunakutana na mataizo mbalimbali ya kijamii likiwemo la ukatili wa kijinsia, ambapo kila kukicha kumekuwa na matukio ya unyanyasaji kwa wanawake.. inasikitisha sana,,

Huko mkoani Kilimanjaro Jeshi la polisi linamsaka mtuhumiwa aliyefahamika kwa jina la Damas pamoja na wenzake watano kwa tuhuma za kumbaka kwa zamu mpenzi wake kisha kumchana na viwembe sehemu za siri.Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Lucas Ng'obhoko amesema mwanamke huyo aliuawa baada ya kwenda kumtembelea mpenzi wake.

Amesema baada ya kufika huko aliwakuta wanaume sita ambao wote walimuingilia kwa zamu kisha kumjeruhi kwa kumchana viwembe. Amesema kwa kuona anazidiwa aliamua kumpigia simu rafiki yake aitwaye Amada na kumueleza mambo yote yaliyompata baada ya taarifa hizo wasamaria wema walijitokeza kisha kumkimbiza hospitalini kwa matibabu na alikufa  muda mfupi wakati akipatiwa matibabu, na wakati tukio linatokea majirani wa wa mtuhumiwa hawakuwepo nyumbani.Kamanda ameliambia gazeti la Alasiri jeshi lake linaendelea na msako  mkali kuwasaka watuhumiwa hao.na maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro.




Picha hizi zinaonyesha wanawake wakiwa katika majonzi wakilia kwa uchungu kutokana na matukio mbalimbali ya kusikitisha..

Huko Pwani pia kuna tukio lakikatili limetokea Mwanamke Siwajibu Omary (45)ameuawa kikatili na mumewe Salum Ally (40) kwa kile kilichodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absolom Mwakyoma amesema tukio hilo limetokea jana saa moja jioni.

Amesema mtuhumiwa huyo alimkatakata kwa panga mke wake  akimtuhumu kuwa anauhusiano wa kimapenzi na mwanamume mwingine.Polisi wanaendelea na Uchunguzi. Maiti imehifadhiwa Hospitali ya Mkoa wa Pwani.Haya matukio yanasikitisha sana jamani sijui tutafika kweli...............



Maoni 2 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

mmhhh mama wee mpaka tumbo laniuma yaani ukatili huu kwa kweli wanawake tunaonewa kweli ni kama vile kiburudisho cha lazima na baadae kukiharibu. Inauma na inasikitisha sana wakikamatwa hao waarifu wapewe adhabu kali sana na waalaaniwe:-( Habari kama hizi zinakasirisha......

Simon Kitururu alisema ...

Inasikitisha sana!:-(

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom