Jumamosi, Novemba 13, 2010

Baba na mama wametengana ni baada ya baba kumkataa mdogo wangu wa mwisho na kusema si mtoto wake,,natamani warudiane sijui nifanyeje...

Kijana huyu anaitwa John a.k.a Makali mkazi wa Yombo  pia ni msanii chipukizi wa Bongo  fleva Dar es    salaam nilikuwa naye katika kipindi cha je wewe ungefanyaje ndani ya studio za Passion fm alikuwa na matatizo yanayohusisha familia alinieleza jinsi ambavyo angependa wazazi wake warudiane "Natamani sana baba na mama warudi kuwa pamoja kwani kutengana kwao kunaleta matatizo katika familia yetu ambapo wadogo zangu bado ni wadogo sana wanahitaji malezi ya baba na mama" alisema John.

Akiendelea kuzungumza kwa uchungu amesema "chanzo cha wazazi wangu kutengana ni baada ya baba kutoka gerezani ambapo alifungwa kwa muda wa miaka mitatu  baada ya kutoka gerezani mama alikuwa na mtoto ambaye ndiye mdogo wangu wa Mwisho baba alikuwa anakataa siyo mtoto wake, hapo ndipo matatizo yalipoanza.Wakati huo wazazi walikuwa wanaishi Rombo na mimi nilikuwa nipo Dar es salaam waliendelea na ugomvi huo ambapo hadi ndugu wa upande wa mama walikuja na kumchukua mama na kumuacha baba akiwa na wadogo zangu".

 Miezi sasa inapita Baba na mama wakiwa wametengana,nijaribu kuzungumza na baba yeye yupo tayari kurudiana na mama na wakayamaliza lakini mama ndugu zake wamemchukua na kumleta Dar es salaam huku wakimshauri asirudiane na baba na kutokana na Mama kujua mimi nataka yeye na baba wapatane alikuja Dar bila kunijulisha na anaishi Kibaha Kwa mjomba na huko Rombo baba amebaki na wadogo zangu"

Kutokana na kuumia sana kutengana kwa wazazi wake kijana huyu ameamua kutunga wimbo akiwaomba wazazi wake warudiane,,inauma sana kuona wazazi wakitengana na mambo ambayo yapo katika jamii yetu kutengana kwa wazazi kunachangia ongezeko la Watoto wa Mitaani na watoto kukosa elimu na malezi bora..unaweza kutoa ushauri wako.

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

pole sana ni party za maisha. nachoona hapa mama anafill shame kwa kitendo alichokifanya. kwa hiyo anakosa amani kuishi tena na baba yako.kama kweli baba amemsamehe jambo ambalo ni ngumu kwa wanaume atafute namna ya kufikisha huo ujumbe wa kumsamehe kwa mama anaweza kurithia akarudi. mjomba hana nafasi ktk mapenzi yao. mapenzi ni kati yao wao wenyewe.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom