Kwa mwanamume ni vigumu kuomba msamaha tena wakati mwingine hubadilisha makosa yao na kukufanya wewe uonekane ndiye mwenye makosa,,,wengine hutumia nguvu kwa kupiga au kununa ilimradi tu kuficha ukweli Kitendo ambacho sio kizuri fahamu kwamba kile ambacho hupendi kufanyiwa wewe na mwenzio hapendi vilevile ushirikiano na heshima ni jambo la msingi. |
Maoni 2 :
Kuna methali moja inasema kila mvuta kamba huvutia kwake, na hata hivyo wahenga wakaongeza nyingine wakisema,asiyekubali kushindwa sio mshindani. Ni bora wanaume wakubali kushindwa kuwa `nisamehe' ni kaluli ngeni mdomoni. Kwasababu gani? mmmh, `udume'
Lakini katika hali yoyote, ili mahusiano, ili maelewanoo yawepo lazima mmoja akubali kujishusha, lakini kama wote mtajiona mafahali basi zitakazoumia ni nyasi, ambazo ni watoto wenu na penzi lenu!
Mkiwa mnapendana, ni vyema mkakubali kuwa kuna `kukoseana' na hili lilitakiwa liwe kwa kila mmoja kwenye nafsi yake, lakini kwa uchunguzi wa dada Adela, wanaume wanakuwa wazito kukubali kukosa na kuomba msamaha! Hii ni kasumba ya `udume'!
Kuna mwenzetu mmoja kasema kuwa mwenye kuharibu mahusiano mema ni wahusika wenyewe, kwa kutokukubali `wadhifa' wa kila mmoja ndani ya ndoa! Huu usemi ukanikumbusha neno kuwa je ulishawahi kusikia bosi akikubali kwa wafanyakazi wake kuwa `nimekosa, nisameheni wafanyakazi wangu' ni mara chache. Hii ni kuonyesha kuwa unapokuwa bosi kwa kasumba, tunakuwa wazito kukubali kukosa, na kuomba msamaha.
Hii ni kasumba, na wakuiondoa kasumba hii ni wahusika wenyewe. Na hili litawezekana kama `mtakuwa karibu ' elezaneni ukweli lakini kwa wakati muafaka, usieleze ukweli huku umevimba kichwa! hapo mtakuwa wote mafahali na mwisho wa siku zitakazoumia nini vile...!
Ahsantu
umenena jambo moja la muhim sn,ni kweli kabisaa hawa wajamaa hata cku moja hawawez kukubali kuwa wamekosa inabidi wabadilike kwakwel maana ipo cku na ss hatutakubali kuonewa ndipo hapo itakapokuwa patashika nguo kuchanika,pale tutakapo sema am done with u kila mtu achukue time yake
Chapisha Maoni