Watoto kama hawa pichani ni watoto ambao wanahitaji msaada kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki ili kuweza kufikia malengo yao,wapo watoto wengi ambao wapo mitaani huku wakiwa wanaishi katika mazingira magumu ikiwa watoto hao ni yatima au sio yatima,, lakini hali duni ya maisha inasababisha ongezeko la watoto wa mitaani na huku watoto hao wakikosa elimu na kujikuta katika hali hatarishi kama kubakwa,kutumia madawa ya kulevya,kuajiriwa katika umri mdogo nk..vipo vituo vya kulelea watoto yatima lakini bado watoto waliopo mitaani wanaongezeka kila kukicha na bila kujua nini hatima ya maisha yao..tusaidiane jamani kwa chochote kwani sisi sote ni ndugu. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni