Mwanamke huyu ni mmoja kati ya wanawake wanaokumbana na matatizo mbalimbali na hivyo kujikuta wakikata tamaa ya maisha.Unyanyasaji wa kijinsia ni matatizo ambayo yametuzunguka sana katika jamii yetu, Kutokana na hali kama hiyo wanaoathirika ni watoto na wanawake, na hivyo kujikuta wakilia na kupata maumivu ya moyo kwa kidonda kisichopona.
Kuna mama mmoja huko Moshi Kilimanjaro anaitwa Mama Joyse ambaye kwa sasa ana watoto watano, katika maisha ya ujana alipatwa na matatizo ya kubakwa na wanaume watano akiwa anaelekea kujitafutia pesa kwa kufanya biashara ya kuuza ndizi, Mama huyo nilizungumza naye akanisimulia tukio lilivyokuwa nilihuzunika sana kiukweli ni hali ambayo wanakumbana nayo wanawake waliowengi ikiwa chanzo ni hali duni ya maisha na mambo mengine mbalimbali. Mama Joyse alisema, Siku ya tukio nakumbuka nilikuwa natoka nyumbani na kwenda kuuza ndizi sokoni ilikuwa ni majira ya asubuhi ambapo mama yangu alikuwa anaumwa amelala kitandani na baba yeye alikuwa hayupo nyumbani ameenda kilabuni kunywa pombe kwani alikuwa ni mlevi na aliisahau kabisa familia, alisema Mama Joyse akiendelea kuzungumza alisema wakati anaenda kuuza ndizi alikuwa amebeba karai na ilikuwa ni asubuhi ya saa 12:30 nilianza safari ambayo ilikuwa ni ndefu sana kwani wakati huo kulikuwa hakuna usafiri maeneo hayo ilikuwa ni mwaka 1989 nilikutana na vijana watano ambao wawili nilikuwa nawafahamu, waliniambia niwape ndizi mimi nilikataa na kuwaambia wanipe pesa kwanza wakati huo walikuwa wamenizunguka ndipo walichukua karai nililokuwa nimebeba ndizi kwa nguvu.
Baada ya hapo wakaniangusha chini na kuanza kunifanyia ukatili huo bila ya huruma huku wakipeana zamu, alisema Mama Joyse kwa uchungu pia alisema wakati huo nilikuwa sijawahi kuwa na mwanamume kwa hiyo kitendo hicho kiliniumiza, na kutokana maumivu makali nilizimia na wenyewe walikimbia na kuniacha, nilikuja kujitambua nipo nyumbani, ndugu zangu waliwatafuta bila mafanikio na hadi leo hii sikuwahi kuwaona tena. Sijui kama wapo hai au la. Inaniuma sana wakati mwingine huwa nikilala tukio hilo hunijia ndotoni ijapokuwa imepita miaka mingi sana lakini sintokaa nisahau hadi kufa kwangu. |
Maoni 3 :
Dada Adela, vitu kama hivi ni rahisi sana kuvisimuliwa, na ni rahisi sana kuviongea, lakini visikupate, kwani vikikupata hutakuwa na maelezo yanayotosheleza. Inamuma na ni donda lisiloponyeka!
Wapo wengi wamekumbana na hayo, na waliofanya hivyo wapo, lakini mimi nina imani kuwa `amfanyiaye mwenzake ubaya kama huo, atalipwa hapa dunia...' Chunguza utagundua hili, waliofanya hivyo wanakutana na adhabu hiyo huenda isipitie kwake moja kwa moja, lakini uchungu ataupata. Wanasema wanaimani kuwa ukimfanyia mwenzako uzinzi na wewe utafanyiwa kama si chumbani kwako ni ubavuni mwa nyumba yako' tafuta tafsiri yake kwa mapana utaielewa vyema.
Lakini kuna mambo mengine tuyatafakari kwa mapana, kuna vitu `vishawishi' kama ilivyoo kachumbari kwenye pilau. Hivi navyo tuviangalie, kwasababu binadamu hatukuumbwa wote sawa, kuna wengine `tamaa zao zamwili ni kubwa kuliko wengine' kuna wanaoweza kuvumilia na kuna amabo hawawezi, labda kwa udhaifu au kwa ujinga! Sasa ni vyema tukachukua tahadhari hasa ya mavazi...kwani hisia unazowatamanisha wadhaifu hao zinaumiza jamii, inaweza usiumie wewe, lakini wakaenda kuumizwa wengine wasio na hatia!
Ni hayo kwa leo
ianasikitisha sana watu kama hao wanaitaji adhabu ya kifo
@Emu three tuko pamoja ndugu yangu nimekubali ujumbe wako@Alice pamoja pia
Chapisha Maoni