Mapenzi ni furaha kama utampata anayekupenda anakujali na kukuheshimu inapendeza kuwa na furaha katika mapenzi ,lakini mapenzi huwa machungu sana pale inapotokea migogoro mbalimbali.
Huko mkoani Ruvuma Mgambo amfumania mke wake akifanya mapenzi na mwanamume mwingine wakati akitokea kusimamia uchaguzi mkuu, akizungumza jana amesema "Unajua nilimuaga mke wangu naenda kusimamia uchaguzi na pengine tunaweza kulala hukohuko,hivyo naye akatumia muda huo kwenda kwa hawara yake akijua mimi sintarudi nyumbani, lakini Mungu ni mkubwa nimefanikiwa kuwafumania ijapokuwa wamenifanyia vurugu ila sintawaachia nitahakikisha haki inatendeka" alisisitiza mgambo huyo.
Amesema hiyo ni mara ya pili kumfumania mke wake ambapo mara ya kwanza alimsamehe na sasa hivi hatakubali kumsamehe badala yake anataka alipwe kiasi cha shilingi 150,000 ili amuachie mke jamaa aliyemfuma, na kwa sasa mwanamke huyo na jamaa wapo kituo cha polisi Mbambabay wakati upelelezi zaidi unaendelea. Duuh mapenzi kizungumkuti. ni muhimu kuwa na uaminifu ili kuepuka migogoro katika mahusiano. |
Maoni 3 :
e bwana we, mambo ya ajabu sometimes japo ya kawaida. Jamani wewe mama umeshindwa nini kuitunza ndoa yako hata ukatulie?
utaula hasara bibiye weweee!
Wakati mwingine watu huwa wanachukua maamuzi ya kuoa/kuolewa wakati hawapo tayari....Sasa mambo gani hayo? mwisho wa siku ni kuleteana magonjwa tuu.
Ukistaajabu ya Musa, utafanya nini vile...?
Chapisha Maoni