Pichani dada huyo unayemuona anaitwa Justina alifika katika studio za Passion fm katika kipindi ninachokifanya cha je wewe ungefanyaje akiwa na matatizo akiomba ushauri kutoka kwa watu mbalimbali.nilizungumza naye akanisimulia mkasa ulivyokuwa"Mimi ni mzaliwa wa Tanga katika maisha yangu niliishi na wazazi wangu baba na mama lakini baadae baba alifariki nikabaki na mama pamoja na wadogo zangu kutokana na hali ya maisha kuwa ngumu sikufanikiwa kuendelea na shule nilishia darasa la saba ili niweze kumsaidia mama kazi za pale nyumbani na baadaye nilitafuta kazi za ndani ambapo nilianza kufanya kazi za ndani nikiwa Dar es salaam.alisema Justina.
Nikiwa naendelea kufanya kazi za ndani nilibahatika kupata mchumba ambaye ndiye mume wangu hadi leo hii mwanzo wa mahusiano yetu kulikuwa na vikwazo vingi kutoka kwa wazazi wangu ambapo walikuwa wakipinga mimi kuolewa na huyo kijana kwasababu walisema alikuwa amezaa na mtoto wa dada yangu kitu ambacho nilimuuliza mchumba wangu lakini yeye alikanusha , basi tuliendelea hivyo hivyo baadae nikaamua kuja kuishi Dar es salaam pamoja na mchumba wangu wakati huo tulikuwa bado hatujafunga ndoa siku zilipita hatimaye nilipata ujauzito na kufanikiwa kupata mtoto baada ya miezi kupita tulifunga ndoa ya kiislamu ambapo kuanzia siku hiyo mimi nilibadili dini nakuwa muislamu.
Hapo ndipo matatizo yalianza kwani mwenzangu tangia nimebadili dini hakuwahi kunipa ushirikiano wowote wa kidini ili na mimi niweze kusali, yeye alikuwa anawasikiliza ndugu zake hata kwa ushauri wowote ambao ninampa mimi anisikilizi hata katika mambo yetu ya nyumbani ni kitu ambacho kinaniumiza sana moyo wangu kwani nilishindwa kujielewa sasa mimi ninayo dini au la kutokana na mazingira kuwa magumu nikaamua kurudi kanisani kusali kumuomba Mungu anisaidie.
Na huko Kanisani mchungaji ameniambia natakiwa nitubu dhambi zangu na baada ya hapo nikisha pata kitubio sitakiwi kuishi na mwanamume labda awe ni mkiristu na niwe nimefunga naye ndoa kanisani na wakati huohuo mume wangu hataki kusikia habari za Kanisani anataka niache na nirudi katika Uislamu na mimi sitaki kwasababu hakuna ninachokijua kuhusu dini hiyo sijui nifanyeje naomba ushauri wenu..... |
Maoni 8 :
Dada Adela hapo ni njia panda kweli kwa dada Justina.! Mi ningemshauri arudi kanisani na amwambie mumewe juu ya uamuzi..Kama atamuacha fine,lakin yeye atakuwa ameiponya nafsi yake inayomhukumu kwa maamuzi aliyoyafanya..Vijana wenzangu tuwe makini na mahusiono tunayojingza, tuchunguzane kwa makin hata familia zetu kama tunaendana..Ahsante n hayo tu.
Kama mdau namba 1 alivyosema. Adela, ur so beautiful. Blog yako ni nzuri sana ila hujaipublish wengi hawaijui. Omba blog maarufu waweke blog yako ktk listi kama 8020, lady jaydee etc
All the best mamii
@Manase thanx ndugu yangu pamoja sana mdau wangu namba mbili
pole ssanna dada yangu ila mi nakuomba kitu kimoja plssss usiende kanisani kwa mungu alishakuongoza kaktka dini sahihi na kaa na mumeo akutafutie mwalimu akufundishe faida ya ndoa ktk uislamu na mumeo pia ajifundishe uislamu hapo mtafaulu.. dahhh inaniuma ssanna kuskia mwanaume anashindwa kumpa maadili ya kislamu mke wake.. dada yangu anakuomba unitumie namba za mume wako nimpe mawaidha na faida za kukuelimisha wewe mke wake dini yako ya hakki.. allah awabariki
una maana gani kuwa mungu kamuongoza kwenye dini sahihi. Ukristo sio dini sahihi? JAMANI KILA MTU AHESHIMU DINI YA WATU WENGINE NA SIO KUONGEA MANENO AMBAYO SI SAHIHI.
Ni kweli kbs aliyosema huyo dada hapo juu ya kua dini ya haki na ya ukweli ni KIISLAMU peke yake.
Ni kweli kbs aliyosema huyo dada hapo juu ya kua dini ya haki na ya ukweli ni KIISLAMU peke yake.
Dada yangu mwangaza umeshakujia katika maisha yako,hakika kua muislamu tambua kama uko katika njia sahihi kabisa,ukweli nasikitika sana mumeo kushindwa kuplay nafasi yake vzr km mume wa kiislamu..nathubutu kusema mumeo ni mmoja kati ya w/me wachache wasiojua majukumu yao na mafundisho ya dini ya kiislamu kwa ujumla..but juu ya yote ayo tambua uyo bado ni mumeo cuz katika maelezo yako hujaoesha km amekuacha..hivyo ushauri wng haina haja ya kurudi kanisani ama kutaka kurudi ktk dini yako ya mwanzo cuz ulipo sasa hivi (kweny uislamu) ni sehemu na dini sahihi mbele ya m/mungu..hilo moja..la pili nenda kwa shehe aliewafungisha ndoa umuelezee kila kitu..ili aweze kuwaita ww na mumeo akupatanisheni na aanze kukupeni mafundsho ya dini ya kiislamu ww na mumeo..ikishindikana basi mtafute shehe yeyote wa kiislamu aweze kukusaidia kutatua tatizo lako...kwakweli roho yng inajiskia uchungu sana mumeo kushidwa kukusaidia kupata mafundisho mazuri ya kiislamu hadi kutaka kufikia uamuzi wakurudi kanisani
Chapisha Maoni