|
Mama Kavishe akitoa tabasamu zito,, thats my mumy nampenda sana sana juzi alikuja kunitembelea na kuniambia maneno mazuri sana, alisema ni Muhimu sana kuwa makini katika maisha ili kufikia malengo yako akasisitiza njia muhimu ni kuwaheshimu wakubwa na wadogo,kumshirikisha Mungu katika kila jambo,kujiamini bila kukata tamaa na pia kuwa na msimamo ni maneno ambayo aliniambia mama na ni vitu ambavyo ni muhimu sana kuvizingatia ili uweze kuishi vizuri na watu wanaokuzunguka |
Pia alisema ni muhimu kukumbuka ulipotoka katika maisha kwani kuna baadhi ya watu wengi wakishafanikiwa basi wanajisahau na kuonyesha dharau kwa watu ambao walimsaidia kwa namna moja au nyingine,,pia alisisitiza kujikubali ni jambo la msingi na kuridhika na unachokipata vilevile kuongeza juhudi katika kazi ili kupata mafanikio mazuri zaidi.TUWAHESHIMU WAZAZI AU WALEZI WETU ILI KUJIFUNZA YALIYO MAZURI KUTOKA KWAO NA KUISHI KATIKA MAADILI MEMA. ASANTE SANA MAMA.
Maoni 2 :
nanukuu "Pia alisema ni muhimu kukumbuka ulipotoka katika maisha kwani kuna baadhi ya watu wengi wakishafanikiwa basi wanajisahau na kuonyesha dharau kwa watu ambao walimsaidia kwa namna moja au nyingine" mwisho wa kunukua:- Ahsante sana mama Kavishe na ahsante Adela kwa kutokuwa mchoyo wa maneno haya ya hekima na busara. Upendo Daima!!
Adela umefanana kweli na Mama yako!
Na asante kwa ujumbe!
Chapisha Maoni