Jumanne, Novemba 23, 2010

Katika maisha ni vigumu kuwa na rafiki wa kweli kama na wewe utakuwa si mkweli..

Nimeipenda sana hii picha wanyama pia wanapenda kuwa na marafiki wa kweli, inapendeza kuwa na rafiki ambaye ni mkweli na muaminifu lakini wakati huohuo tukumbuke huwezi kuwa na rafiki mkweli wakati wewe ni muongo. Imekuwa ikitokea marafiki wengi kuwa maadui kutokana na migogoro ya aina mbalimbali na migogoro hiyo mara nyingi ikihusishwa na pesa, mapenzi, majivuno,umbea nk.


Watoto pia huweza kuwa marafiki wazuri lakini vilevile huwa inatokea wanagombana na kujikuta wanakatisha urafiki wao kutokana na ugomvi wa aina mbalimbali ila huwa ni rahisi watoto kusameheana  pale wanapogombana  na kuendeleza urafiki wao


Urafiki wa wanawake unaweza kuwa ni urafiki mzuri sana kama wote mtakuwa ni waaminifu kwani mara nyingi wanawake kinachosababisha kukosana ni umbea,mapenzi nk inawezekana mwanamke kuwa na rafiki mwanamume na urafiki wao ukawa mzuri kuliko urafiki wa mwanamke na mwanamke ambapo mara nyingi wengi wao wanakuwa ni wanafki na mwisho wake kukosana na kuendeleza dhana ya kwamba wanawake hatupendani.



Mnaweza mkawa mnakula kunywa na kucheka pamoja na hivyo usigundue kama rafiki yako ni adui yako. NI MUHIMU KUWA WAKWELI NA WENYE MSIMAMO ILI KUDUMISHA URAFIKI WA KWELI HAIPENDEZI KUWA RAFIKI MNAFIKI.


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom