Ijumaa, Desemba 10, 2010

Je inawezekana kupangiana zamu ya kupika na kazi nyingine za ndani kwa wanandoa

Mwanamume akiwa anaanda chakula,wapo wanaume ambao wanajua kupika na wanapenda kufanya hivyo kwa matakwa yao binafsi na si kulazimishwa ni ajabu kumkuta mwanamke amekaa huku akimpelekesha mume wake kufanya kazi za ndani,, Imetokea kuna jamaa mmoja analalamika mke wake anataka wapangiane kufanya kazi za ndani kwa madai kuwa anachoka sana kwani hata yeye yupo bize na kazi na yote ni kutokana na mwanamume kukataa kuajiri msaidizi wa kazi za ndani,,,je ipo sawa hii

Maoni 7 :

Bila jina alisema ...

Sio kwamba kwasababu mimi ni mwanaume basi naamua kutetea upande wetu, sio sawa kabisa kupangiana kazi kwa watu walioana especially kazi za ndani, haisound kabisa hata kwa nyie wanawake ujikalishe tu wakati mumeo anafanya kazi za ndani, otherwise mwanaume awe ameamua tu kufanya hizo kazi kwajili ya kumuonesha mkewe kuwa anampenda lakini sio kinyume na hapo

Simon Kitururu alisema ...

Asilimia 90 % ya wapishi wazuri DUNIANI -(Nazungumzia upishi babukubwa na sio ilimradi kuwa na chakuliwa) Ni wanaume.

Cheki hoteli babu kubwa, Ikulu karibu zote DUNIANI na hata kwenye KICHENI PATI BONGO utaafikiana na mimi kuwa WANOGESHAO msosi ni WANAUME.

Turudi kwenye mada:
Kwa wanandoa kupangiana zamu inawezekana.



......tatizo ni kwamba TAMADUNI,mila na USHAMBA ....kwa kawaida hasa kwenye mpangilio wa KAZI kitamaduni hasa AFRIKA na hata Marekani KUSINI na ASIA ,......



.... kazi ya kupika ilikuwa ya MWANAMKE kwa kuwa ndiye aliye kuwa anakaa nyumbani kulea watoto na kutunza nyumba.

Lakini katika dunia ya SASA ambayo kuna uwezekano MKUBWA TU ni WANAWAKE wengi ndio wenye mshahara mkubwa na waendao kazini muda mrefu,...
...mwanamume anaweza kupika kusaidia na sio tu kuonyesha ajuavyo shughuli kuliko mke wake akiajiriwa kuwa mpishi wa hoteli ,IKULU, kwa KIMADA au tu MSIBA wa JIRANI.:-(


Nawaza tu!:-(

Bila jina alisema ...

ni kweli wapo wanaume wanapenda sana kupika, wengi ni wale walioendelea, nakumbuka nikiwa mdogo tulikuwa tunaishi ndani ya yard wizara ya ujenzi Rukwa, yupo jirani yetu alikuwa reginal Engineer, alikuwa na mke mabinti, housgel, lkn cku moja 1 alikuwa akipika, yani msosi hasaa.

pia Moro Mkaka m1 alikuwa ameishi USA for long tym, alikuwa akipika sana, na bila uficho nawaambieni yapo baadhi ya mapishi nilijifunza toka kwake.

lkn wanaume wengine huwa wanajfeel inferior kupika, au hata kusaidia kazi yoyote ya ndani. ni vema waondokane na hayo mawazo potofu. maisha kusaidiana jamani

Bila jina alisema ...

wengine wameathiriwa na mila na desturi za kwao. km uchagani,usukumani,ukuriani, c rahisi mtoto wa kiume kukaa jikoni, kuosha vyombo nk. labda hawa waliokulia mjini.

Bila jina alisema ...

yes ofkoz km wote ni wafanyakazi na hawana msaidiz ni sawa kabisa mwanaume kumsaidia mke wake kazi za nyumban koz wote wametoka kutafuta na wamechoka..zile enzi za kufanyana watumwa zimeshapitwa na wakati ss

emu-three alisema ...

Wanasema kuta za nyumba huficha mengi, na mengi tunayonena mdomoni huenda kabisa yasiwepo ndani ya kuta hizo. Yupo jamaa kijiweni kwetu hupenda kuwasaga wanaume wanaowasaidia wake zao kazi za nyumbani kama kupika kuosha vyombo nk. Jamaa huyu tuliamini hivyo kwani anaongea kwa jaziba na kusema wafanyao hivyo ni waume bwege.
Siku moja tukamtembelea nyumbani kwake kwa kumshitukizia, tulipofika tukamkuta mke wake anasoma gazeti na huku television inaonyesha mchezo wa kuigiza wa akina Majuto.
Mwanamke yule alitukaribisha na alionekana kukunja uso , na akatukaribisha kiti. Tulimuuliza mumewe yupo wapi:
'AAh, yupo nje, tangu jana maviombo yapo nyorodoo, na ilikuwa zaumu yake kuosha,...subirini kidogo kwani nikimpa mwanya ataondoka na maviombo yatadoda tena..' akasema huku kakunja nne anaangalia runinga. Tulitizamana tukacheka.
Baadae jamaa akaingia akiwa kavaa bukta, kajaa machafu ya vyakula mkononi, alipotuona akarudi nyuma na kutokomea nje alipokuwepo, alirudi baadaye kavalia nguo za kawaida.
'Du, mbona mumekuja ghafla, nilikuwa nafanya usafi wa bustani nje kidogo...siunajue tena mume ukiwa nyumbani kuna kazi mama anazisahau, bustani...mmmh'
'Na kuosha vyombo...' akamalizia mke wake
Ninachotaka kusema ni kuwa haya yapo lakini kwa mpangilio mliokubaliana. Inawezekana kama kwa mfano wote ni wafanyakazi, ...hata hivyo mila na desturi zetu ni muhimu kuzingatiwa! Tusije tukafanya `kukomoana' ili kuleta usawa, hapana. Mke ana sia zake na mume ana sifa zake, tusije tukaamua kuiga hata yale ambayo yanampa mke wa kiafrika sifa zake, kwani mwishoo wa siku tutakuwa kama jamaa yetu huyo!

Bila jina alisema ...

inawezekana endapo wanandoa wenyewe watakubaliana kwa sabababu ni jambo la kawaida katk maisha!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom