Jumatano, Desemba 22, 2010

Kuna umuhimu wa kukaa na kutafakari juu ya uhusiano ulionao kwa yale uliyopitia kabla ya kuuanza mwaka mpya.


Mapenzi bila kuwepo maelewano baina ya wapendanao basi hapo hakuna mapenzi, na katika safari ya mapenzi ni vizuri kwa wapendanao  kupata muda wa kuzungumzia juu ya uhusiano walionao walipotokea na wanapoelekea kuangalia malengo mliyokuwa nayo nk..na pia kwa yule ambaye mwaka huu ulikuwa ni wa matatizo sana katika suala la mapenzi ni muda wako kutafakari nini kilisababisha kuwapo na matatizo hayo na kujua nini cha kufanya ili kuanza vizuri mwaka mpya na kama kuna makosa yalijitokeza na bado ulikuwa na kinyongo ni vizuri kusameheana na kuanza upya kwa amani na upendo kuna mengi sana yanayotukia katika safari ya mahusiano ikiwa ni kwa wachumba na walio kwenye ndoa yapo yaliyokufurahisha na yapo yaliyokukera, ni muhimu kutafakari ili kuwa na uhusiano imara na wa kudumu.

Maoni 1 :

emuthree alisema ...

Ni kweli Adela, kama watu watafanya hivi kwenye ndoa zao, hata kila jambo kukaa na kutafakari badala ya kukimbilia kulewa eti wanashukuru kumalaiza mwaka ingekuwa mswano.
Ikifika saa sita sijui ile mnakaa mnamshukuru mungu, manapiga mahesabu mnatazama wapi mlikosea, manasameheana na mnapeana mapenzi mazuri ya kuanza mwaka, na wanasema watu kuwa ile saa yA mwanzo lile utakalo lifanya la mwanzo litaleta baraka au kinyume chake. KWAHIYO Nawashauri wanandoa ile saa, au dakika za mwanzo, kwanza mshukuruni mungu na pili peaneni mapenzi mazuri, kauli nzuri furahini kama vile mpo kwenye honeymoon! MTAONA JAZA YAKE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom