Alhamisi, Desemba 23, 2010

Hivi ni kwa nini katika maisha baadhi ya watu wanapokosea huogopa kukosolewa ikiwa ni kazini,nyumbani na hata shuleni.


Wanasaikolojia wanasema mtu mwenye tatizo la kutojikubali na kujiona yeye ni duni ni mgumu sana kukubali kukosolewa watu wengi kama si wote hawapendi kukosolewa bali hupenda kuambiwa kwamba walivyofanya ni sawa na kwa yule ambaye hajiamini kitendo cha kukosolewa hukiona kama jaribio lililofanikiwa na kubaini udhaifu wake na ndio maana si rahisi kwa mtu huyu kukubali kukosolewa, kutokana na kushindwa kujiamini na hivyo akikosolewa anakuwa mkali na mwenye kuona aibu....mimi naamini hakuna binadamu aliyekamilika kwahiyo inapotokea umekosolewa katika jambo fulani basi jaribu kusikiliza ili ujue namna ya kujirekebisha na hata yule anayemkosoa mwenziye ni vizuri akatumia njia nzuri ya kumkosoa na si kwa kumkejeli au kumsimanga kwa kumuona hawezi Tusaidiane katika kila jambo.


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom