Alhamisi, Desemba 23, 2010

Swali kutoka kwa James mkazi wa Mwanza,,nimeishi na mke wangu miaka mitano nimegundua mtoto tuliyenaye si wa kwangu nataka nimuache.,,,

Migogoro katika mahusiano kama uonavyo pichani hao ni baadhi ya wapendanao wakigombana mbele ya mtoto,,Jamani uwanja wa mapenzi una mambo mengi James mkazi wa Mwanza amenitumia ujumbe na kusema ameishi na mke wake yapata miaka mitano sasa amegundua mtoto aliyekuwa akimlea si wa kwake anasema,,,siku moja nilikuwa nimetoka kazini kufika nyumbani mke wangu alikuwa ametoka akawa ameicha simu yake chumbani nikiwa naendelea na kazi zangu mara ujumbe ukaingia katika simu ya mke wangu ule ujumbe ulikuwa umetumwa na mwanaume ukisema. ,,,nimechoka kusubiri ninachotaka ni mtoto wangu vinginevyo nakuja kumwambia ukweli mume wako,, haya maneno yalinichanganya alisema James aliporudi mke wangu moja kwa moja nilimuonyesha ule ujumbe na kutaka anieleze ukweli nilikuwa mkali akaanza kulia huku akiniomba msamaha na kusema ni kweli kuwa mtoto si wa kwangu ni wa boyfriend wake wa kwanza ambapo mimi nilipomuoa tayari alikuwa na mimba bila ya mimi kugundua ananiomba nimsamehe kwani bado ananipenda sana,,, lakini mimi moyo wangu haupo kabisa nahisi kumchukia sana yeye pamoja na mtoto nawaza kuwafukuza maisha yangu naona hayana amani wazazi bado hawafahamu lolote naomba ushauri kwa watu mbalimbali

Maoni 4 :

Martin K alisema ...

Hii kali sana adela, I mean unaweza kufa kama hujui kushikiria moyo! kwakweli mi nampongeza James hajachukua maamuzi mabaya yoyote. Unajua kuna kitu mimi huwa najiuliza, je nini kibaya kataka maisha ya binadamu, kumbe nahisi majibu sina ila kila kitu unachokifanya kinyume na utashi wa binadamu mwingine ni kibaya, kifanye akiwa anajua au ameamua kukuacha ufanye japo kuwa hakuungi mkono. Huyu Dada kakose tena sana; kwa upande mwingine ni muuaji, kwa kuwa kuna watu wana hasira mbaya sana angeweza kuuawa au kusababisha mtu afe kwa ugomjwa wa moyo. na huyu kaka naye vile vile kitendo cha kumuacha wakati huyu dada bado anampenda ni kibaya, akumbuke kuwa huyu dada huenda alimpenda japokuwa alikuwa kwa bahati mbaya kapewa ujauzito na mtu mwingine aliamua kukaa kimwa. Ushauri wangu ni kuwa James aangalie ni lipi zito, Je akimuacha ana hakika ya kupata copy ya huyo, akiwa na morphology kama ya huyo, upendo, upole ukari tabia njema ama mbaya kuvumilia kushauri kusistiza kama huyo atakayemwacha? kuna wasichana wazuri kwa sura na umbo tunawafahamu, wanatembea hata na waume za watu wanajinyenyekeza mpaka basi wakiwa nje ya ndoa, ngoja waingie sasa utajuta! vile vile afikirie je yeye hata umia moyo na mengine mengi na cha msingi tu amrudishe mtoto kwa baba yake kwa ridhaa ya mama yake ili asikae akaaumia akimuona huenda na muda alioopitisha bila kuwa na mtoto wa kwake mwenyewe ni mrefu mno miaka 5, anatafakari sana ahsante
Martin K. Dodoma

Simon Kitururu alisema ...

Labda kuna la kujifunza kutoka kwa wanao ADOPT watoto ambao hawakuwazaa wenyewe na kuwalea kama wanao wakuzaa.

Kitu ``Mtoto wangu ´´ mara nyingi ni cha kisaikolojia zaidi kwa kuwa mara karibu zote siri ya baba ya mtoto ajuaye ni MAMA ya mtoto na BAB ya mtoto kimfarijicho ni imani tu tu mtoto ni wake.


Na katika swala hili MTOTO naye akumbukwe kuwa yeye hana makosa na ni athari gani atapata kwa ghafla afikiriye kuwa ni BABA akigeuka sio BABA.


Swala gumu hili na lahitaji ujasiri sana na labda hakuna mwenye jibu SAHIHI asiye kwenye viatu vya wahusika ndani ya tatizo hili.:-(


Nawaza tu kwa sauti!:-(

emuthree alisema ...

Siri kubwa ya ndoa ni kuaminiana, kuwa wakweli , na hili ni bora lianzaie mapema. Wapo wameolewa au wameoa, wakiwa na watoto tayari, na walikwua wawazi kwa wapendwa wao, na wakakubaliana hilo.
Kama una mwenzako ana mambo ya chinichini, anakuficha baadhi ya mambo na unakuja kuyagundua baadaye mahusioano yenu yana walakini.
Lakini Suluhisho sio kukimbilia kuachana, au kugombana, ni kukaa pamoja na kijadili, kuwa kosa limetokea, na mejeraha nimepata,majeraha haya tutayatibu vipi, je mwenzangu umefanya hili kosa, una mipangilio gani, maana isije ikawa mwisho wa siku mkawa na mahusiano ya chinichini tena na kubandikwa mtoto mwingine. Na ikibidi muiteni huyo mwenye mtoto muwekane sawa, kama anauwezo wa kumlea basi mpeni huyo mtoto, lakini kuwe na makubaliano yaliyo mema.
Kuna jamaa alisema kuwa siri za watoto anayejua ni mama, huwezi jua unalea watoto kumbe sio wako, na una uhakika gani huyo utakayepata baadaye kakamilika...swali kubwa la kujiuliza wanandoa ni kuwa je tunamdanganya nani...tukumbuke kuwa haya tutendayo leo yanajirudia, kwa kizazi chako, je utafurahi mtoto wako afanye au afanyiwe kama wewe.Kama unaipenda familia yako na maisha yao ya baadaye jirekebishe na omba msamaha, muanze maisha upya!

Bila jina alisema ...

ukimuacha haisaidii kitu

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom