Jamani moyo huwa unapenda sana lakini wakati mwingine unakuta unapenda sehemu ambayo hakuna furaha mfano unakuwa na mpenzi kwa miaka mingi kama mitatu hadi mitano lakini siku zote huwa anakuumiza kwa matukio tofauti akikusaliti na wewe binafsi unajikuta unamsamehe kila kukicha kwasababu unampenda je kweli ni sawa kufanya hivi coz sometime uvumilivu jamani una mipaka yake............ |
Maoni 9 :
Kupenda sio mchezo dada Adela, wapo watu wanapigwa na kutolewa ngeu lakini hawaachani. Yupo dada mmoja alikuwa kila siku kipigo kwa mumewe, mlevi, na siku moja akapigwa mpaka akazimia na kutolewa ngeu, na kuvunjika mguu, akarudi kwao, na wazazi wakampiga marufuku kurudi kwa mumewe, lakini binti alipopona huyooo akatoroka na kumrudia mumewe.
Nasikia baada ya tukio hilo mumewe ameanza kujirudi. Hili ni kusema, wakati mwingine ni ibilisi, na mnapo-oana mjue mumekuwa kitu kimoja, huenda fujo, ulevi vuruguu ni kitu kidogo kipo kichwani kwa mumeo, tafuta dawa, na umsaidie ili umuokoe, sio kumkimbia.
Ukimsaidia utakuwa umemponya au sio, ila ikizidi omba ushauri, ikishindikana akili kichwani mwako!
unajua mapenzi ni kitu cha ajabu sana1 ndo maana wanafalsafa wanasema mapenzi ni upofu pia mapenzi kizunguzungu yaani ukipenda kwa kumaanisha alafu mwenzako akawa anabeep huwezi amini akikutenda, akikurudia tena ukakubali unafikiri amekuwa serious lakini mapenzi bana mmmmhhh........
mi nadhani ni kutojiamini kwa watu wengine wanapigwa na kudhalilishwa lakini wanaendelea na mausihano kwa hofu ya kutotongozwa tena au kupata watu wengine wa kuwapenda tena.Na wengine wanavumilia yote haya kwa sababu muhusika akiondoka financially hawataweza kusimama.NI KUTOJIAMINI NA KUSHINDWA KUSIMAMA KWA MIGUU YETU BILA KUMTEGEMEA MTU.
Kipenda roho, na nakubaliana na waliotangulia mapenzi, upendo ni kitu cha ajabu sana.....
Adela, ni kweli haya yanatokea na mara nyingi wanawake hufanyiwa hivi wakavumilia na kurudi kwa mwanaume anayewanyanyasa time and again. Mi nilishapitia abusive relationship kila nililokuwa naambiwa na kuona mwenyewe nikifanyiwa nilivumilia, ukweli ni kwamba nilivumilia kwa miaka 6 nikitegemea mwenzangu atabadilika, hakubadilika na mwisho nilisema inatosha na nikaondoka. Ni wachache sana wanaweza kutoka kwenye hizi abusive relationship wengi huishia kufa aidha kwa msongo wa mawazo au kipigo.
Sijaelewa ni kwanini kwasasa nimeingia kwenye abusive relationship nyingine, ila ukweli ni kwamba mapenzi huwa yanaoungua taratibu na mwishowe huisha kabisa mnabaki kama kaka na dada. Huu uhusiano niliokuwa nao sasa mwannzoni hata kulala nilikuwa silali kwa kumuwaza sasa hivi hata nisipomuona siku 2 wala sishtuki.... Najua tu nao utaisha kifo cha mende. Sitaulilia kwani 'doesnt worth my tears'. wanawake tuamke na tukubali kuachia pale inabidi kuachia, mwanaume akiamua kukuacha dakika moja wala hageuki nyuma sisi tunashindwa nini?
na pia wanawake wengi tu wanapenda mashindani km rafiki yake kaolewa au kachumbiwa na yeye atajitahidi mpaka apate mwanume hata km hampendi utakuta mwanaume anamtenda hana raha kwenyi relationship lkn anamganda mwanaume ili na yeye awe na wake utakuta hana raha lkn anamganda mwanaume kwa kujionesha na kutaka kujiprove for her self i have a man anafikiri kapata kumbe kapatikana watu km hawa wanasikitisha sana penzi halina shaka wala mateso ila wanawake wengine sijui ni malezi wanapenda kuteswa na mwanaume eti vumilia mtu akutenda ww bado tu umemganda km hakupendi na kukuheshimu hata ukimzalia hatakuheshimu wasichana wasikuhizi wanashida na wanaume inasikitisha sana na mwanaume anajua kwamba demu kaniganda ndio anatake advantage.
daaah kiukweli inauma sana jamani mimi huwa nawaza kama ingelikuwa ni yeye angejisikiaje coz kumuumiza mwenzio ni kitu kibaya sana ila kutokana na mapenzi aliyonayo bado anabaki anakugana kwa kufikiri utabadilika lakini unakuta hakuna mabadiliko hali ni ileile i hate this jamani
It Pains Adela
kiukweli unakuta wanawake wengi tunapenda kiukweli kiasi cha kwamba hata ukiingia kwenye mahusiano na uakawa unaumizwa kuacha mara moja ni kazi unajitahidi kuvumilia ukiamini siku moja atabadilika kumbe kwa mwenzio ni tofauti
Chapisha Maoni