Jumanne, Januari 04, 2011

"baada ya kutoka safari nimekuta Kaka yangu anataka kufunga ndoa na mchumba wangu"anaomba ushari Baraka wa Dar es salaam

Ama kweli kwenye mapenzi kuna mambo jamani nimepata ujumbe huu kutoka kwa Baraka "Nilikuwa na mchumba wangu kwa muda wa miaka mitatu na wakati wote kaka yangu alikuwa akimfahamu sasa ilitokea mimi nikapata safari kwenda nje kikazi kwa muda wa mwaka mmoja nikiwa huko tulikuwa tunawasiliana vizuri tu na mpenzi wangu tatizo limekuja wakati niliporudi na kukuta mikakati ya harusi ya aliyekuwa mchumba wangu na kaka yangu kiukweli imeniuma sana kiasi kwamba najihisi naweza kufanya chochote kibaya kwani nikimuuliza mwenzangu kwa nini amefanya hivyo ananiambia amejikuta anampenda sana kaka yangu na huyu kaka yangu tumechangia baba  ila mama tofauti namchukia sana kwa sasa inaniuma sana na sijui nifanyeje................

Maoni 3 :

Kitomai alisema ...

Hiyo mbona imetokea kwa mtu ninayemfahamu. Jamaa kachukua girl friend wa kaka yake kamuoa na sasa ana watoto naye wawili.Unajua mwili ni mali ya mtu binafsi kwa sababu hiyo anaweza kumgawia mtu yeyote amtakaye. Ukilijua hilo utakua mpole. Hupo hapo sister Adela. Huyo Baraka kama shida yake ni mwanake kuna maelfu ya wasichana wako tayari kwa ajili yake tena huenda wakawa na sifa zaidi kuliko hata huyo.

emuthree alisema ...

Hapo shukuru mungu na wape baraka zote, najua inauma sana, lakini hebu fikiria ungemuoa na hawo watu wakawa wanapendana kisiri ukaja kugundua ingekuwaje. Hapo mungu kakusaidia kayaweka mambo hadharani, Muombe mungu, vuta subira, na mwisho utapata aliye chaguo lako na la mungu na utasema aheri ningelijua hili mapema. Warembo wapo wengi, na wanazaliwa wengi, achana na huyo, na wala usimchukie kaka yako...!

Bila jina alisema ...

Hello!!!!!
Sorry my dear ndio dunia naungana na huyu emu-three , hapo juu! Mshukuru Mungu kwa hilo. Da Adela kama una contacts za huyu kaka please may I have it please! Thanks again!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom