Alhamisi, Januari 20, 2011

Inakera sana mwanamume kutoka usiku na kumuacha ndani mwenza wako akikusubiri tena inawezekana umeondoka hata bila ya kuaga na simu umezima.

Huwa inauma sana unakuta mwanamume yupo na marafiki zake au popote pale anapopajua yeye huku amemuacha mwenza wake akiwa mpweke bila ya kuaga na wakati mwingine unakuta simu amezima hali hii husababisha migogoro katika mahusiano na tabia hii ipo sana kwa wanaume kurudi usiku wa manane na akiulizwa kuwa ametoka wapi? anakuwa mkali na wakati mwingine kama amelewa mwanamke anaweza akapigwa au kutukanwa  bila kosa lolote


Jamani mimi  nauliza baadhi ya hao wanaume wanaofanya hiyo tabia hawajisikii vibaya au JE KAMA INGELIKUWA MWANAMKE NDIYE ANARUDI USIKU WA MANANE UNGEJISIKIAJE  NI MUHIMU KUTAFUTA FURAHA NA SI KERO KATIKA MAPENZI...


Maoni 4 :

Bila jina alisema ...

jaman hawa wanaume zetu ni pasua kichwa acha tu akiwa bado ajakupta anasumbua unamuonea uruma akikupata ata mda wa kukujali unaisha cjuwi kwa nn jaman.

emuthree alisema ...

Hilo ni kosa, tatizo kubwa ni kusahau `majukumu ya ndoa, na pia kutokuua misingi ya ndoa...'
Jamani ndoa ni raha, ndoa nisehemu ya kutuliza akili...sio baa, sio nanihino...

ADELA KAVISHE alisema ...

tuko pamoja ndugu zangu tatizo ni kujisahau na hivyo kupelekea hali kama hiyo kutokea lakini mimi naamini inawezekana mtu akajirekebisha kwa kujitambua kile anachomfanyia mwenziye siyo sahihi

Bila jina alisema ...

Kuan upande wa pili wa hili Adela. Wanawake wengine wana gubu, maneno yasokwisha, ugomvi hata hujui unapotokea. Ukirudi tu toka kazini kosa, hata kupumzika huwezi ni hili na hili na hili. Basi wanaona bora wakapumzike huko wakirudi wanalala tu.
Wanawake nasi tujue jinsi ya kuongea na wenzi wetu. Mambo mengine yananoga na yanasikilizwa zaidi yakisemwa mahala pale pa raha.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom