Huwa inauma sana unakuta mwanamume yupo na marafiki zake au popote pale anapopajua yeye huku amemuacha mwenza wake akiwa mpweke bila ya kuaga na wakati mwingine unakuta simu amezima hali hii husababisha migogoro katika mahusiano na tabia hii ipo sana kwa wanaume kurudi usiku wa manane na akiulizwa kuwa ametoka wapi? anakuwa mkali na wakati mwingine kama amelewa mwanamke anaweza akapigwa au kutukanwa bila kosa lolote |
Maoni 4 :
jaman hawa wanaume zetu ni pasua kichwa acha tu akiwa bado ajakupta anasumbua unamuonea uruma akikupata ata mda wa kukujali unaisha cjuwi kwa nn jaman.
Hilo ni kosa, tatizo kubwa ni kusahau `majukumu ya ndoa, na pia kutokuua misingi ya ndoa...'
Jamani ndoa ni raha, ndoa nisehemu ya kutuliza akili...sio baa, sio nanihino...
tuko pamoja ndugu zangu tatizo ni kujisahau na hivyo kupelekea hali kama hiyo kutokea lakini mimi naamini inawezekana mtu akajirekebisha kwa kujitambua kile anachomfanyia mwenziye siyo sahihi
Kuan upande wa pili wa hili Adela. Wanawake wengine wana gubu, maneno yasokwisha, ugomvi hata hujui unapotokea. Ukirudi tu toka kazini kosa, hata kupumzika huwezi ni hili na hili na hili. Basi wanaona bora wakapumzike huko wakirudi wanalala tu.
Wanawake nasi tujue jinsi ya kuongea na wenzi wetu. Mambo mengine yananoga na yanasikilizwa zaidi yakisemwa mahala pale pa raha.
Chapisha Maoni