Ijumaa, Januari 14, 2011

Inauma sana unapogundua rafiki yako anakusaliti na mpenzi wako,,

Katika maisha tunaishi na watu wa aina mbalimbali na wenye tabia tofauti inapotokea unaye rafiki yako iwe ni mwanamke au mwanamume ambaye unamuamini kwa kila kitu  kama rafiki lakini ikatokea siku akakusaliti kwa mpenzi wako na kuamua kutoka naye kimapenzi kiukweli huwa inauma sana na wengi inapotokea hali kama hii huwa wanachukua maamuzi tofauti ikiwa ni pamoja na ugomvi,,kuachana nk.lakini pia yupo yule ambaye anaweza kusamehe na kuendela na maisha yake kama kawaida .,Chanzo katika hili kikubwa ni tamaa zisizokuwa na maana na zinaweza kuzuilika.HAIPENDEZI NA SI VIZURI KUTOKA KIMAPENZI NA MPENZI WA RAFIKI YAKO NI MUHIMU KUSTAARABIKA JAMANI

Maoni 2 :

emuthree alisema ...

Wahenga wanasemaje `KIKULACHO KINGUONI MWAKO'

Simon Kitururu alisema ...

Inasemekana KIKULACHO kwa kawaida ki NGUONI mwako!

Na akujuaye ndiye mara nyingi awezaye kukusaliti!:-(

Lakini ndiyo hivyo ,...
...MAPENZI ni USINGIZI ,...
.... na wengi huzinduka usingizini na kuanza kufikiria baada ya kitendo kikishatendeka.:-(

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom