Ijumaa, Januari 14, 2011

Mimi ni mwanamume mpenzi wangu wa zamani anahatarisha maisha yangu naombeni ushauri..


Sina shaka unaendelea vizuri na majukumu ya ujenzi wa taifa hususani kuelimisha na kusaidia jamii yetu ya kitanzania. nitafurahu kama jina langu utaliweka kapuni utapo itoa habari hii,nahitaji msaada wa wadau kimawazo na ushauri kwani nipo katika wakati mgumu sana.
 Nilikuwa na mpenzi wangu ambaye sikubahatika kuwa naye karibu kwa kipindi kirefu kwani nilipata nafasi ya kwenda nje ya nchi masomoni kwa muda wa miaka mitatu na hata sasa bado nipo huko,mwanzo ulikuwa mzuri kwani tulikuwa tukiwasiliana na kupeana moyo lakini baada ya muda alibadilika na kuwa mkali ,akinitolea maneno ya kashifa na kulifaninisha penzi letu na jehananu kwani halina faida bali ni kuongeza stress tu. Sikuona taabu sana japo nilimpenda lakini ilibidi niachane nae na kuendelea na maisha yangu mengine na pia kupata mpenzi mwingine ambaye tunapendana sana na kuheshimiana.
Mpenzi wangu huyo wazamani alipata taarifa za mimi kuwa na mpenzi mwingine na hapo ndipo taabu ilipoanzia kwani amekuwa akifanya visa vingi sana, ametafuta namba zangu za simu na za mpenzi wangu wa sasa na kuwa akituma  ujumbe wa matusi na majigambo,sasa imefikia wakati anafanya vurugu hata kwa wadogo zangu na kuwatumia watu wa kuwafanyia vitu vibaya.Kila kunapokucha anatafuta jinsi ya kutugombanisha.
 Sasa wadau ndugu yenu sina amani na pia maisha yangu,mpenzi wangu na wadogo zangu yapo hatarini mnanishauri nifanyeje? mnanishauri nifanyeje

Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

Waambie wadogo zako wakaripoti polisi hapo hatawasumbua tena, kwa upande wenu msimjibu msg kabisaaa, hata akitukana vipi kaeni kimya atachoka tu

emuthree alisema ...

Kuna usemi usemao, ukikikosa utakijutia, ukiwa nacho hikina maana sana. Ndivyo tulivyo, wanadamu!

Bila jina alisema ...

mpotezee tu huyo hana maana, amefulia hana jipya. concentrate na maisha yenu na kwa sasa simu zimesajiliwa kama anatukana mpeleke polisi na ashitakiwe kwa mujibu wa sheria. Alikataa kwa nini wakati wenzake wanajiuliza watakipata lini, tena mtu mwenyewe uko MAULAYA watu tunaota tuu. Go on with your life.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom