Kuna neno moja ambalo baadhi ya watu huwa wanalitumia katika mahusiano inawezekana mwanamume au mwanamke akawa haonekani nyumbani mara kwa mara labda kutokana na kazi au mambo mengine binafsi sasa kutokana na hilo ikatokea siku moja mwenza wako akaamua kukaa na wewe ili kuzungumza na kukueleza hivi " mpenzi wangu unajua nakukosa sana kila siku unachelewa kurudi hatupati hata muda wa kukaa pamoja nakuwa mpweke sana" na jibu likawa hivi "lakini mpenzi mimi mbona huwa silali nje kila siku narudi nyumbani tena tunalala kitanda kimoja na tunakula pamoja sasa unanikosa kivipi" kiukweli mimi sizani kama kulala pamoja na kula pamoja inatosha kuwa karibu na umpendaye ni lazima utafute muda wa kuwa unakaa na mpenzi wako kwa mazungumzo mengine ya kifamilia nk, kama utatoka naye out au utakuwa naye hapohapo nyumbani kwani kuna watu ambao huwa hawashindi majumbani mwao kila siku anarudi usiku wa manane,,,,,HATA KAMA KAZI ZIMEKUBANA LAKINI KUMBUKA PIA UNA DENI LA KUWAKARIBU NA UMPENDAYE PALE UTAKAPOPATA NAFASI |
Maoni 3 :
Ni kweli ni muhimu na sio tu pale upatapo nafasi inabidi kuitafuta kwa nguvu!! Ahsante kwa ujumbe huu wa ijumaa hii.
Naaam
Kuna mengi mema ya kujua kuhusu mapenzi na mahusiano.
Lakini hii mada ya mahusiano ni PANA kuliko mahusiano yenyewe. Mwisho wa siku, narejea kufunza niliyofunzwa kuwa SIRI YA MAFANIKIO YA NDOA / MAHUSIANO, HUBAKI KUWA SIRI
Blessings
Fanya ufanyalo lakini ukumbuke kuwa `majukumu ya ndoa ni lazima' ikiwezekana kama mwenza kakuita ilii kuyatimiza hayo majukumu, muombe bosi wako ruhusa, kwani `hilo utaulizwa, kwanini ulikataa wito wa ndoa...' lakini isiwe na mazoea..lol
Chapisha Maoni