Unajua katika mapenzi unaweza ukaishi na mtu akakupa tabu sana,ila uvumilivu ni kitu cha busara,kwani inawezekana akakusumbua sana,akukera kutokana na mapungufu yake ya kibinadamu lakini bado unahitaji kuendelea kuwa naye maana licha ya kukukera ,ila anakupenda kwa dhati. kumbuka kuwa uvumilivu ni nguzo ya pekee ili tuweze kufika mbali katika mahusiano ukizingatia kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha. |
Maoni 2 :
Tatizo watu wengi hawaongelei matatizo yao kitu kifanyacho kuwa bonge la kazi kustukia kiini cha mapungufu na kutibu hayo mapungufu!:-(
Hata gilasi kabatini hugongana sembuese sie wanadamu. Mnapokoseana ambizaneni na sameheaneni...!
Chapisha Maoni