Inapotokea migogoro wengine hutengana na kujengeana chuki,lakini wapo wale walioachana bila ya kinyongo na katika hili inategemea nini kilichosababisha mkaachana ,kitu ambacho ni kibaya zaidi ni ile hali ya wapendanao wanapogombana kidogo kwa kosa ambalo wangeweza kukaa pamoja na kutafuta ufumbuzi lakini inakuwa tofauti na kukuta mmoja kati yao anaanza kumzungumzia mwenzie vibaya na kutoa siri za ndani nje kwa mfano unakuta mwanamke anamzungumzia vibaya mwenza wake kwa maneno ya kashfa mbele ya marafiki zake au majirani lakini baada ya siku mbili tatu unakuta bado yuko pamoja naye sasa hali kama hii siyo nzuri kwasababu haimzalilishi mwenza wako peke yako bali wote kwa pamoja......KUWA MAKINI KUTOA SIRI ZA NDANI YA PENZI LENU HAIPENDEZI. |
Maoni 2 :
Yaani, ulijuaje Adela. Nina rafiki yangu tena wa karibu juzi kanipigia simu amechanganyikiwa. Ana girlfriend wake ni kama wanaishi pamoja kimtindo kwani binti anasoma chuo kikuu hivyo weekend hivi, sikukuu na wakati mwingi hana vipindi anakuwa kwa mshikaji. Si wamegombana kidogo tu, binti kaja juu kabeba kila kilicho chake halafu kaanza kumtukana mwenzake matusi makubwa ya nguoni kwa nguvu mpaka watu wakajaa, jamaa uvumilivu ukamshinda si akampiga. Wakatulia kidogo, mara simu ikaita...he binti akaanza kumwambia aliempigia, eeh nakuja ndio, yaani anavyoongea kama vile huyo anayeongea nae anajua kila kitu kuhusu mahusiano yao na alimpa ushauri wa kuachana. Ajabu, baada tu ya wiki keshaanza kuomba msamaha arudi kwa mshikaji.....awww!
Kwahiyo, nakubaliana na wewe kabisa kuwa migogoro ndani ya uhusiano hupelekea hayo lakini wengine tunajiendekeza. Mlianzana kwa heshima basi kuachana kusiwe sababu ya kuachiana makovu yasiyo na sababu.
@Mdau hapo juu tuko pamoja sana kiukweli inaumiza na mwingine anafanya hivyo akifikiri atapata ushauri mzuri kwa wale anaowasimulia kumbe wengine wanamcheka
Chapisha Maoni