Jumatano, Februari 09, 2011

Fahamu sikukuu ya valentine ilipoanzia.

Sikukuu ya wapendanao inasherekewa kila ifikapo tarehe 14 mwezi wa pili kila mwaka.
Watu wengi wanaosherekea siku hii kwa Nchi za Afrika Mashariki ni vijana walio kati ya miaka 18 hadi 35.
Historia ya sikukuu hii inaanzia miaka mingi jijini, Roma, Italia ikiwa inahusishwa na mtakatifu Valentine au Valentinus aliyekuwa akiishi jijini humo katika karne hiyo. Wakati wa maisha ya mtakatifu Valentine Roma ilikuwa ikitawaliwa na Kaisari, Claudius II, ambaye alipata hisia wakati huo kuwa askari mkakamavu na bora zaidi ni yule asiyekuwa na mke wala familia .Claudius alilifanyia kazi wazo lake na aliamua kupiga marufuku ndoa zote kwa askari wa nchi hiyo, jambo ambalo halikukubaliwa na mtakatifu, Valentinus. Hivyo Valentinus alichukua jukumu la kukaidi amri ile na kuendelea kuwafungisha ndoa kwa siri maaskari waliokuwa wakitaka kufungishwa ndoa.
 
Haikuchukua muda mrefu, taarifa zilimfikia mfalme, Claudius na alipopata habari hizo aliamuru kukamatwa na kufungwa gerezani na kisha Valentinus aliuawa kwa amri ya Kaisari. Kuna taarifa zinadai kuwa kabla ya kuuawa kwa Valentine wakati huo akiwa amefungwa, mtakatifu Valentine aliandika barua ya salamu kwa binti aliyekuwa amekwenda  kumsalimia gerezani. Na mwisho wa barua kulisomeka maneno yaliyoandikwa ‘From your Valentine.’
Tangu hapo Valentine akawa anakumbukwa kama mtetezi wa wapendanao na siku hii ikawa inaadhimishwa duniani kote.
Baada ya kufariki kwa mtakatifu huyo ndipo wananchi wengi duniani wakaamua kuadhimisha siku hii kama sherehe ya kumkumbuka Mtakatifu Valentinus.

Maoni 1 :

emu-three alisema ...

Duuh, kumbe kuna maswala ya `imani' ndani yake sio `malovu hisia' pekeee!
Nashukuru mpendwa; Niliadimika kidogo hapa kwako, siunajua tena, ukipiga hodi mara kadhaa kwa mwenzako, akawa haji kwako, au anakuja na kusalimia nje, inabidi na wewe umuige...lol
USIJALI TUPO PAMOJA!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom