Katika kusherekea sikukuu ya valentine kuna waliofurahi na kuna waliolia jamani nimepata ujumbe huu kutoka kwa mama Salma akisema mimi ni mwanmke nimeolewa nina watoto wawili nimeishi na mume wangu kwa miaka sita sasa nimegundua kuwa anatoka nje ya ndoa ni baada ya kumkuta akiwa na zawadi za Valentine kutoka kwa mwanamke mwingine, zawadi hizo alikuja nazo nyumbani huku akisema kuwa mimi ndiye niliyemtumia hizo zawadi akiwa kazini lakini mimi sikuwa nimefanya hivyo kwani nilikuwa nimemuandalia zawadi palepale nyumbani, kibaya zaidi yeye anakataa na kusema labda hizo zawadi aliyetuma amekosea sio za kwake kiukweli mimi inaniuma sana kwani nimeshindwa kumuamini hata akiwa anajitetea ninachoamini najua ananidanganya kwani tokea nimkute na hizo zawadi amekuwa hana amani kabisa, naombeni ushauri kwani nilikuwa namuamini na kumpenda sana mume wangu ila kwa sasa nahisi kumchukia simuamini tena.
Maoni 12 :
Pole mama Salma, mi nakushauri hivi, kama kweli hizo zawadi hajui zimetoka wapi na anakazania ni wewe umemtumia. Na kama anajali/kinamuuma jinsi gani hizo zawadi zimeleta kutokuolewana/kasheshe kwenye ndoa. Basi akukabidhi hizo zawadi ili either ukazichome au ukazitupe jalalani na hapo itakuonyesha kuwa hazijali na hajali nani kamtumia. Lakini akizingangania basi dadangu ujue anakudanganya.
Haya maisha ya ndoa bwana basi tu.
mh inawezekana kweli mme wako hajui nani amemtumia dada yangu. usichukulie hatua za harakaharaka wengine wanataka kuharibu tu ndo za watu. labda kuna mdada amempenda akaona amtumie zawadi na kwa sababu yeye hana mtu mmwingine akaona moja kwa moja aje nazo nyumbani akijua ni mkewe amemtumia. kama angakuwa na mtu mwingine angasita hata kuja nazo huko nyumbani kwa sababu hazina jina kwamba zinatoka kwa nani. usimchukie bure na kujenga uhasama kwenye ndoa na mmeo. jaribu kuchunguza, asante
Inawezekana kweli kaletewa na mwanamke ambaye hana mpango nae,kama angekuwa ni mke wake asingeleta kukuonyesha.Wewe muamini tu mumeo ila uendelee kumchunguza siku hadi siku,kwasababu wanaume hawaaminiki na pia usije ukamuamini mwanaume yoyote kwa asilimia zote kuwa hatoki nje, wapo lakini ni wachache, hivyo wala usipoteze furaha yako bure kwaajili ya upuuzi huo, muombe mungu awe kinga yako tu.
Angekuwa mwanaume gani awe na kimada aliyemtumia zawadi halafu azilete home?? Kuna uwezekano mtu kamchenga tu.Na kama vipi kwa nini ajichongee kihivyo?Huyo alieyezituma amejifurahisha mwenyewe bila shaka anammendea mumeo lakini amekwama na kuishia kutuma zawadi bila kujitambulisha.
Acha kulalamuka moyoni mwamini mumeo, na ukinza kumjengea mashaka ndoa yako itakuwa hatarini sana maana mumeo atakuwa na amani kabisa lakini wewe utaishia kufanya mawindo yasiyo na mnyama wa kumkamata.Unaposema amekosa raha si kweli hizo ni hisia zako tu.Na labda anawaza nani kamchezea hiyo rafu ya kumkosanisha na wewe.Mwamini mumeo asilimia zote usimfanyie mawindo utaja umbuka mwenyewe.
Jmani mme wako ni mkweli kwani angejua zimetoka wapi asinge kuja nazo home , muamini tu na umpende kama kawaida.
mapenzi ni pamoja na kuaminiana mwamini mumeo huenda ni kweli kabisa kaletewa hivyo usimfanye akajisikia vibaya hata kama hana aende kutafuta jaribu kumuonyesha umemuamini na eaenjoy zawadi atajiju aliyejipendekeza. mradi alirudi nyumbani na mkawa wote hicho ndicho kikubwa, wengine walirudiwa siku ya 2.
Just be careful ma friend Mungu wetu ni wa ajabu hujui anataka kukuonesha nini kuna mawili kajisahau kaja nazo au kuna ibilisi kwy mbo la mwanamke anania ya kuharibu ndoa yenu . Be careful just forget but have a sceptical mind
man are very good in drama, hizo zawadi amepewa na kimada wake, kajichomoa akili na kuja nazo home akiwa tayari amejipanga ataongea nini ndo maana amekuwa mkavu like he dont knw watsup...bt am telling you just mkabidhi kwa Mungu yy atakupigania koz huwezi jua kuumia kwako kama hata kuna affect what he is doing...be happy mumy mkabidhi Mungu matatizo yako atakupigania we mwenyewe utashangaa...show him more love FORGIVE AND FORGET HAYO MAMBO YAPO SISI BINADAMU WPYE NI WADHAIFU mpenzi, tc
Miaka sita ya ndoa ni balaa mwanawane. Hata mimi mume wangu alikuwa mwaminifu nilidhani nimeolewa na malaika. Ilipofika miaka sita nilijuuta kumfahamu. Ila huyo kimada nilimtia adabu mume wangu kwa sasa anamkodolea kwa mbali tu.
Jamani nisaidieni na mimi hiv mme wangu atakuwa anatoka nje au vip?nimekuta sms kwenye simu yake kutoka kwa mwanamke nanukuu mwanamke:beb uko wap?mwanaume :niko tanga.siku nyingine mwanamke:mpenzi vp?uko wap?mwanaume :niko hospital wife mgonjwa.mwisho wa nukuu.nilipatwa na baridi ya ghafla nilipomuuliza alidai ni mwanamke anaemsumbua mda mrefu,na mimi sikutaka kumwamini nilimpigia huyo mwanamke nimeweka loudspiker nikamuuliza anauhusiano gan na mme wangu hakutaka kuniambia nikamwambia awe mbali na mume wangu akacheka kwa kejeli akaniambia atajitahidi.jamani niko njiapanda anachoniambia mme wangu nimwamini au ni hawala yake nisaidieni.nataka nimfanyie kitu mbaya huyo malaya coz anajua mme wangu ameoa.
Mimi nniadhirika kisaikolojia kiukweli inaniuma nimeshindwa kuamini tena mme wangu takriban miaka 10sasa ninachoamini amenidanganya kwani aliondoka nyumbani aliporudi nilikuta manii katika nguo zake za ndani nikamuita nakuuliza je nini hiki asema hajui wala hajuii ninkitu oooh kweli imeonekana mme wangu anatoka nje ya ndoa kweli nimeendelea kumbembeleza aniambie ukweli ushahidi ninao nimfanyajeee
Nimechoka natabia hiii namkomeshaje nimechoka sio mara moja zaidi ya mara 4 sasa anasingizia vitu ambavyo havifananiii sasa inatosha pia niwazi kwamba hata kinga hatumii ataniletea magonjwa hajali
Chapisha Maoni