Kuna baadhi ya watu ambao wapo katika mahusiano kwa muda mrefu ikatokea wameachana labda inawezekana kuna sababu zilizowapelekea kutengana kama migogoro ya hapa na pale nk lakini pia kuna ile hali mwanamume au mwanamke anatengana na mpenzi wake huku akiulizwa sababu anasema tumeachana tu hakuna sababu ila ni uamuzi waliofikia, embu fikiria mwanamume au mwanamke uliyekuwa unampenda sana siku moja anakuita na kukuambia hivi ,,mimi na wewe tumekuwa pamoja kwa muda mrefu nilikuwa nakupenda sana lakini kwa sasa naona bora tuachane na tuwe marafiki pia naomba usinifikirie vibaya ni moyo wangu umeamua hivyo kwamba hatuwezi kuendelea kuwa wapenzi,,,, haya ni mambo ambayo huwa yanatokea katika baadhi ya mahusiano mtu unampenda unamuamini lakini anakuja na maneno kama hayo na kwa wakati huo wewe bado unampenda nini cha kufanya hapa wadau,,je ni kweli inawezekana wapenzi kutengana bila sababu................ |
Maoni 4 :
Haiwezekani kuachana bila sababu!
Na ukisoma hata kwenye kilichoandikwa hapa - na nukuu:
``kuna ile hali mwanamume au mwanamke anatengana na mpenzi wake huku akiulizwa sababu anasema tumeachana tu hakuna sababu ila ni uamuzi waliofikia, embu fikiria mwanamume au mwanamke uliyekuwa unampenda sana siku moja anakuita na kukuambia hivi ,,mimi na wewe tumekuwa pamoja kwa muda mrefu nilikuwa nakupenda sana lakini kwa sasa naona bora tuachane na tuwe marafiki pia naomba usinifikirie vibaya ni moyo wangu umeamua hivyo kwamba hatuwezi kuendelea kuwa wapenzi,,,,´´-mwisho wa nukuu.
- utastukia kuwa kuna sababu HAPO hata wakati mtu anadai HAKUNA SABABU na kirahisi ni kuwa PENZI limekufa na mtu hampendi tena mwenzie kimapenzi.
Na mimi naamini haiwezekani kulazimisha penzi na dawa ya kutibu kuachika ni kukubali kuwa PENZI limekufa na kuanza kivyako na MUDA hutibu . Na kwa kuwa BINDAMU tuko wengi atatokea tu mtu mwingine mbele ya safari ya maisha ambaye unampenda na yeye anakupenda.
Na kufa kwa penzi ni jambo la kawaida - tatizo ni maadili ya jamii yageuzayo kuwa ni jambo la ajabu na kufanya watu wengi hasa wailiooana kushindwa kuachana kwa kuogopa kuhukumiwa na jamii kama watu wabaya.
NI MTAZAMO wangu tu huu!
Inawezekana kuchokana bila sababu ktk ndoa au relashionship ya muda mrefu sana.mazoea ya sana interest inaishi mnajikuta u r mates not lovers anymore mwisho mnachokana au hata maudhi madogo madogo in some point yanakuja kuwa chanzo cha kuachana utamvumilia mwenzio lkn kunasiku moja unajiuliza kwanini niteseke au niumie ndio unakuta couples wanachana bila sababu
@Anony: Mbona nikikusoma naona sababu nyingi tu unazieleza kwanini WATU wanaachana?
Bado naamini lazima kunakuwa na sababu tu.
Kwa mfano kutoka kwenye komenti yako:
-mazoea ya sana interest inaishi mnajikuta u r mates not lovers
-maudhi madogo madogo in some point yanakuja kuwa chanzo cha kuachana
-utamvumilia mwenzio lkn kunasiku moja unajiuliza kwanini niteseke
-utamvumilia mwenzio lkn kunasiku moja unajiuliza kwanini niumie
Hizo zote ni SABABU.
Kwa hiyo bado nashangaa unapomalizia sentensi na:
-unakuta couples wanachana bila sababu .
Nafikiri wengi wafikiriao watu huachana bila sababu ni tafsiri zao tu za sababu ambazo hufanya wasistukie kuwa kuna SABABU zinazofanya watu kuachana hata wale wadaio kuwa wameachana bila sababu.
Ni mtazamo wangu tu huu!
Nakuunga mkono Mtakatifu., Kuachana bila sababu haiwezekani....... Lazima kuna sababu kuna wengine husema..... sisi wenyewe tulikuwa tunapendana ila wazazi ndo walituachanisha... sababu ni wazazi hapa sio....
Kwamaana hiyo sababu za kuachana lazima ziwepo, yawezekana wewe uliyeachwa usiikubali sababu aloitoa mwenzio kuachana na wewe, lakini bado twarudi palepale sababu ipo.
Kuna binti mmoja aliachwa na bwanaake kisa mchafu, wacha aje juu sababu gani hiyo unayoniachia una nyingine wewe sio hiyo, huyo ukimuuliza sababu za kuachana na mwenzie atakwambia hata hakukuwa na sababu.
Hata mapenzi huanza kwa sababu iweje yasiishe kwa sababu? Iwe ndogo, kubwa justifiable of not, still sababu huwepo.
Chapisha Maoni