Katika mapenzi hali ya kuachana au kuachwa ni jambo ambalo linaweza likatokea katika uhusiano ulionao usipokuwa makini,,na chanzo cha wapenzi kuachana mara nyingi hutokana na migogoro,,uongo, na mambo mengine mengi hali hii inapotokea watu wengi hukata tamaa katika mapenzi na kujikuta wakisema "sintokaa nipende tena katika maisha yangu" au nawachukia sana wanaume au wanawake ikiwa aliyemtenda ni mmoja,,mimi naweza kusema kwamba inapotokea umeachwa au umeachika ni vizuri ukatulia na kutafakari na baadaye kuanza maisha mapya huku ukiwa na malengo mazuri na pia ikitokea umepata mchumba basi kuwa makini ili isije ikatokea unaachwa tena kwani matapeli katika mapenzi ni wengi na hata hivyo inawezekana wewe pia ukawa una matatizo ambayo yalipelekea ukaachika hivyo ni vizuri ukajitambua na kuanza maisha mapya,,,,USIJIUMIZE KWA KUKATA TAMAA LIPO CHAGUO LAKO MUHIMU KUWA MAKINI
Maoni 2 :
Mimi naamini:
Katika mapenzi hali ya kuachana au kuachwa ni jambo ambalo linaweza likatokea katika uhusiano ulionao HATA UKIWA MAKINI.:-(
Na hata uwe makini vipi ,...
...UMAKINI wako bado UTAKUWA TU unaudhaifu wa KIBINADAMU ambao labda hata binadamu mwingine pembeni yako umdharauye kwakuwa kwa umakini wako unadhania yeye ndiye siye MAKINI ,...
...anauona hata wakati uko BIZE unafikiri kila ufanyalo halinakasoro kwa kuwa mtu unajiamini WAKATI HUO na katika PENZI HILO uko MAKINI.
Na ndio maana wengi wafikiriao wanafanya kila kitu sawa na wanaamini wanampagawisha mtu hushangaa wakitemwa au kustukia wafikiriaye wanampagawisha anakula uroda sana tu na HAUSIBOI au HAUSIGELi wakiondoka pichani baada ya kufikiri washashibisha penzi.
UMAKINI kwa bahati mbaya kipimo chake hakina UJAZO mmoja kwa kila mtu !
Na LABDA mwisho wa kuacha na kuacha ni KIFO cha BINADAMU mhusika!:-(
Nawaza tu kwa sauti!:-(
Kwakeli Adela, inauma mwisho wa kuuma, ila tukumbuke kuwa kila kitu hutokea ili iwe sababu, huenda kuachana huko kukawa na heri ndani yake, lakini kwa udhaifu wa kibanadamu hatuwezi kujua. Bora kweli uwe mvumilivu, ili usije ukaruka mkojo ukakanyaga...
Chapisha Maoni