Jumatatu, Machi 21, 2011

Maneno ya watu yanaweza kuwa chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano ya walio wengi

Inawezekana wawili wanaopendana kugombana kutokana na maneno ya watu,,mara nyingi katika hili inategemea maneno hayo yanaweza kuwa na ukweli ndani yake au yasiwe na ukweli wowote,, kwani naamini mtu anapokuletea maneno kuwa mpenzi wako anakusaliti ni muhimu ukatulia na kuchunguza ukweli uko wapi bila ya kukurupuka sasa waliowengi huwa wanakurupuka na kujikuta wanakatisha mahusiano waliyonayo kwa maneno yasiyo na ukweli fanya uchunguzi kwanza kabla ya kuchukua hatua yoyote.......

Maoni 3 :

Simon Kitururu alisema ...

Tatizo mapenzi mengi,...
.... muonekano wa wengi hata katika kuvaa,....
..... mpaka wajuayo wengi ,...
... yana misingi mingi muhimu ambayo inatokana na wafikiriavyo wengine wanawaza nini.


Kwa hiyo kama mtu kuanzia nguo avaazo , achanavyo nywele, MPAKA ni kwa nani anajipendekeza inatokana na maneno ya watu au tu afikiriayo ni maneno na wafikiriavyo watu wengine,...


... nadhani unaweza kuona ni jinsi gani kukurupuka na kujikuta unakatisha mahusiano uliyonayo na MTU ilivyo rahisi.:-(


Watu wengi maana ya MAISHA waishio huletwa na wasikiayo na wafikiriayo wengine wanasema nini kwahiyo kama kunuka kikwapa chako ukiwa peke yako hakikusumbui ila mbele za watu kinakusumbua na unahitaji deodorant au pafyumu,...
... naamini kirahisi unasikiliza ya watu na ukisikia ya watu uwasikilizao hata umbeya kuhusu LIMPENZI lako ,...
... hata ujifanye humaindi ,...
... kiaina fulani ushaathirika na kama ni muwekaji tamutamu karibu na sehemu zake za viungo vya siri baada ya kusikia umbeya hata bila kutaka unaweza kujikuta pua zako unajaribu kuzifanya zistukie kama kuna harufu tofauti na uliyoizoea kwenye viungo hivyo vya siri ambavyo zamani ulikuwa huvinusi kihivyo.:-(

Nawaza tu kwa sauti!:-(

emuthree alisema ...

Uaminifu katika ndoa ni muhimu, na uaminifu ukikosekana ndio chanzo cha kusikiliza umbeya. Ukumbuke kuwa sio wote wanaowatakia heri katika mahusiano yenu. kwahiyo basi, kitu cha kwanza jenga uaminifu kwa mwenzako, na umwamnini yeye kwanza, ....ndio baadaye uchuje hayo yanayoletwa na wengine.
Tukumbuke kuwa mnapooana mnakuwa mwili mmoja, sasa kweli wewe mwenyewe waweza kufanya hayo unayoambiwa kama `umbeya'...? Kama una tabia hiyo basi cha muhimu ni kujirudi!

Bila jina alisema ...

Ukifanya maamuzi yako ya kumuacha mpenzi wako eti tu kwa maneno ya kusikia basi utakuwa huna msimamo. Maneno ya kuambiwa tizama na ukweli ulivyo/umjuavyo mwenzio na utafiti uwepo kabla hujaamua vinginevyo utaachana na kila mtu...
Pia ukumbuke hata huyo partner wako labda anaambiwa kuhusu wewe pia, je naye akuache kwa kusikia??
ukisikia, fanya utafiti, uliza na ongeeni na kisha amua.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom