Inawezekana waliowengi katika mahusiano ya kimapenzi hawapendi kuwa wazi katika hili,,ikiwa ni katika hali ya kuridhika kwa yale yanayofanyika kwa mfano tabia za mwenza wako, kama ni mtumiaji kilevi, hajipendi yaani mchafu,nk kama haujaridhika na tabia hizo ni vigumu kuwa na uhusiano ulio na furaha ndani yake, na pia inawezekana tabia hizo ambazo haujaridhika nazo ni mbaya na unaweza kumsaidia mwenzio akajirekebisha katika tabia hizo ili muende sawa, vilevile kuna hali ya kutoridhika katika tendo la ndoa ambapo husababisha mwanamume au mwanamke kutoka nje ya ndoa kitu ambacho sio sahihi kama unaona mwenzio hakuridhishi kuwa muwazi. JAMANI UKIMYA HAUJENGI BALI UNABOMOA NI VIZURI WOTE MKARIDHIKA NA KUWA NA FURAHA YA KUDUMU MILELE. |
Maoni 1 :
Mnapooana mnakuwa kitu kimoja, inakuwaje wanandoa mnajigawa vipande, hivi kweli inawezekana, upande wa kushoto wa mwili ukawaza hili na upande mwingine ukawaza vingine?
Tuwe wawazi ili kudumisha ndoa, ukiwashwa sehemu mwambie mwenzako nawashwa hapa nikune!
Chapisha Maoni