Alhamisi, Machi 17, 2011

mimi ni mwanamke inaniuma sana nimemfumania mpenzi wangu na rafiki yangu'''

Habari yako Adela pole na majukumu ya kazi mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 27 nipo katika mahusiano kwa takribani miaka sita nilikuwa nampenda sana mpenzi wangu na tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa hivi karibuni, nilimuamini na kumuheshimu ila tatizo nimegundua kumbe alikuwa akinizunguka na kutembea na rafiki yangu baada ya kufanya uchunguzi nimegundua yote haya na kwa sasa tupo katika ugomvi kwani nimeumia sana lakini bado nampenda ila nikifikiria kilichotokea kwamba alikuwa anatoka na rafiki yangu roho inaniuma sana na yeye mwenyewe amekiri kosa na kusema ilitokea bahati mbaya na anasema kuwa ananipenda,, na yule rafiki yangu baada ya kufahamu kuwa mimi nimegundua ukweli sijawahi kumuona hadi leo hii naomba ushauri kupitia blog yako sijui nikiendelea na huyu mwanamume atanitenda tena kwani nahisi kuvunjika moyo na kukata tamaa.

Maoni 3 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Kwa mtindo huo naona hakukupenda kwa dhati kama ulivyompenda wewe. Hata kama amekiri ni mara moja ilikuwaje yeyey anafanya uchumba na wewe na huku anatembea na rafiki yako na wote wawili wanajifanya kama hakujatokea kitu? kAMA ILIKUWA BAHATI MBAYA BASI ANGEKUJA KWAKO NA KUKUAMBIA KUWA HAYA. Lakini amesubiri mpaka wewe umegundua..... mimi ningemwcha na huyo rafiki yako si rafiki wa kweli kabisa...haya ni mawazo yangu..

Simon Kitururu alisema ...

Kama sababu iliyofanya aonje nje wakati yuko nawe mara ya kwanza bado ipo !

Basi atafanya tena tu!

Na sababu ni nyingi,...
... ikiwa ni mpaka self esteem yake au hata tu nini anakikosa kwako ambacho kinamfanya afikirie kuonja nje.


Fikiria nini kimebadilika kwenye mahusiano yenu sasa hivi ambacho kinaweza kumtuliza ndani na kama hakuna basi akipata nafasi ataonja tu nje angalau kwa siri mpka umdake tena.


Tafakari sana jambo kwa kuwa watu wengi vigumu huwa ni kufanya kitu kwa mara ya kwanza tu -KUGUMU ni kuonja tu kwa mara ya kwanza au hata kuiba tu kwa mara ya kwanza lakini akishafanikiwa kuondoa bikira ya wizi,....
...kurudia wizi ni mteremko sana kwa wengi na hufanyika tu bila hata kujisikia vibaya.:-(!

Ni mtazamo tu !

Bila jina alisema ...

IS JUST MAWAZO YANGU BELIEVE ME OR NOT KAMA USINGEJUA ANGEENDELEA SANA PLUS UPO NAE KATIKA RELETIONSHIP KWA MIAKA SITA UMEKUJA KUGUNDUA NOW POSSIBLE AMEKUCHEAT KWA MUDA MREFU,SIKILIZA MOYO WAKO NA UCHUKUE UAMUZI WA MAANA USITAZAME SIJUI UMEISHI NAE MIAKA SITA LIFE INABADILIKA UNAWEZA KUMPATA MWINGNE AKAKUHESHIMU HATA KAMA HAUPO AROUND SIO HUYO ANAYEPATA UPENYO KIDOGO TU UKAUTUMIA NA RAFIKI YAKO,TO BE HONEST THINK SANA HATA KAMA UNAMPENDA PLZ,,,NI HAYO TU

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom