Nimepata ujumbe kutoka kwa Tina mkazi wa Dar es salaam, Naombeni ushauri jamani nina mpenzi wangu tupo kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja na tuna malengo ya kufunga ndoa na kuishi pamoja sasa kinachonishangaza ni kwamba mpenzi wangu anasema eti nipate mimba kwanza halafu ndiyo tufunge ndoa, mimi nilimjibu na kusema kwa nini tusifunge tu ndoa kwani kama ni mtoto tutampata hata tukiwa ndani ya ndoa,,alichonijibu ni kwamba hawezi kunioa kabla sijapata ujauzito vinginevyo kutakuwa hakuna ndoa kiukweli nimekaa na kutafakari sana kama kweli anavyoniambia yeye yuko sahihi au hanipendi nia yake ni kuangalia kama mimi nitapata mimba au la naombeni ushauri wadau kwani nawaza bila ya kupata jibu................ |
Maoni 6 :
very complicated kwa kweli lakini ushauri wangu kwa huyo dada ni hivi
kiukweli jamaa anaweza akawa anampenda tena sana ila kuna uwezekano kukawa external force kutoka nje ya mahusiano(shinikizo ) either kwa ndugu au marafiki hilo moja .
2)yawezekana jamaa nia yake ni mtoto tu na si vinginevyo kama kweli anampenda na wana malengo hawezi mshinikiza mwenzie kwani kufanya ni kwenda kinyume na madili ya kidini na jamii yetu kwa ujumla
chakufanya sasa huyo dada akaze moyo konde na yeye amshinikize wawe wachumba kama hawaja ili waweze tambulika kwenye familia sidhani kama wakiwa wachumba itakuwa shida
Je kama asipopata huo ujauzito itakuwaje, hebu kwa nyongeza ya hili wasoem hikii kisa :
http://miram3.blogspot.com/2011/03/maisha-yana-kila-aina-ya-mitihani-1.html
kiukweli dada ndoa ni sheria mtoto ni majaliwa ina maana hata akikuoa ukakosa mtoto atakunyanyasa achana nae hakupendi huyooooo ! yeye anafanya mtoto ni sheria wapi nawapi ! kama umesikia haya kama wewe ni king'ang'anizi haya utakuja kuniambia siku moja huyo hata ukipata watoto wapi hatakupenda mtu anaekupenda hana sharti lolote itakavyokuwa anakuhitaji wewe sio watoto wakija poa
huyo c,o mhohaji ila anataka mtoto toka kwako
Kama mnafuatilia ndoa zilizo nyingi sasahivi biharusi anakua tayari ana Mimba.sisemi na nyie ndio lazima mfate hio no lkn kama hayo ndio matakwa yake!!.Cha msingi kwakua hatujui hatua mlioyofikia mfano engagement na vitu kama hivyo ni vema mkafanya hivyo kabla ya yote ili familia zenu ziwe kama back up coz wapo wanasema ubebe mimba then ukibeba ana kumwaga.
Kiukweli ni masharti magumu na ya kiunyanyasaji lakni ndio hivyo wanasema mtaka cha uvunguni sharti ainame.Pengine hana uhakika kama una uwezo wa kuzaa of which kama utaolewa nae halafu hauzai utanyanyaswa hii ndio picha halisi uliyopewa intro kwamba ubebe mimba kwanza jamaa hataki kuuziwa mbuzi kwenye gunia!
mwenzangu we yasije kukukuta yaliyonikuta mie hapa, niliambiwa hivyo hivyo na bwana hadi wazazi wa bwana kwamba nizae kwanza ndo niolewe basi uzazi wangu ulikuwa wa shida nilitafuta mimba mpaka jasho lianitoka siku ya siku mimba nimepata na kuniacha akaniacha. ila nashukuru nimebaki na kopi yake(mtoto).
Chapisha Maoni