Alhamisi, Aprili 21, 2011

Je unaamini kuwa mwanamke anaweza kuwa chanzo kikuu cha kuzeeka au kuchokana katika mapenzi???

Ni wazi kuwa katika mahusiano wapendanao hupitia vikwazo mbalimbali hivyo bila ya kuvumilia hatua hizo mwisho wao unakuwa mbaya, hatua ya wanandoa kuchokana  inasababishwa na wanandoa wote wawili kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya haki za mume na mke  kumbuka utulivu huzaa mapenzi na huruma  baina ya wanandoa, wataalamu wanakuambia mwanamke ana nafasi kubwa ya kujenga au kubomoa ndoa na hii haina maana kwamba mwanamume hana nafasi ya uharibifu bali nafasi ya mwanzo inachukuliwa na mwanamke bila ya upinzani, mambo ambayo yanasababishwa na mwanamke na kuwa chanzo cha kuchokana katika mapenzi ni pamoja na kuzoeana baina ya wanandoa jambo ambalo ni zuri lakini linaweza kuwa baya kama litatumika vibaya na kupelekea kuleta dharau ndani ya nyumba hasa kwa upande wa mwanamke kwa kutojali usafi wake wa mavazi anayovaa, chakula anachopika nidhamu ya nyumba na mpangilio kwa ujumla

Kwa mfano enzi za mwanzo wa ndoa mwanamke huwa anajali sana usafi  wa mwili wake, umaridadi wa nguo anazovaa, upishi wa chakula unaozingatia vionjo na ubunifu , mapokezi yenye bashasha lakini baada ya kuzoena yote hayo yanabadilika mwanamke huhisi hana jipya la kumuonesha mumewe hujiona wameshakuwa watu wazima na maranyingi utakuta mwanamke huyu anashinda na sare moja kuanzia asubuhi hadi anapopanda kitandani usiku mambo ya aina hii yanachangia kuhatarisha uhai wa ndoa.Haipendezi kujisahau hadi kufikia hatua ya kuifanya nyumba yako kuvurugika ni muhimu kujitambua na kujikosoa pale unapokosea..KUMBUKA KUJISAHAU KWA WANANDOA NI TIKETI YA KUTENGANA.

Maoni 1 :

Simon Kitururu alisema ...

Adela umenidaka kwa sana hapa``....hatua ya wanandoa kuchokana inasababishwa na wanandoa wote wawili kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya haki za mume na mke...´´

Leo chichemi zaidi!:-(

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom