Jumanne, Aprili 19, 2011

Maandalizi ya Ndizi mshale na nyama ya ng'ombe

Mahitaji ya pishi hili ni pamoja na ndizi mshale kiasi unachopenda kulingana na familia yako, nyama ya ng'ombe  nusu kilo vitunguu maji vikubwa viwili nyanya moja pilipili hoho moja, karoti moja, mafuta ya kupikia kijiko kikubwa kimoja na chumvi kiasi..Jinsi ya ya kuandaa na na kupika anza kwa kuosha nyama vizuri na katakata vipande vidogo unavyopendelea na kisha chemsha hadi iive.Nyama yenye mafuta kidogo na mifupa kidogo inafaa sana kwa ndizi, kisha menya ndizi zako vizuri na kuzikata katikati kwa urefu na kisha kwa upana (msharazi) kisha zioshe na kuweka kwenye sufuria yenye maji masafi.
Hivi ni viungo unavyotumia,katakata vitunguu,nyanya karoti na pilipili hoho halafu chukua sufuria ya kupikia na weka ndizi kiasi kisha weka nyama na supu  yake na vitu vyote  ulivyokatakata weka pamoja(vitunguu, nyanya,hoho na karoti)Kisha  weka na ndizi zilizobaki kwa juu
Hakikisha supu uliyoweka inatosha kuivisha ndizi  kama ni kidogo sana ongeza maji ya moto na pia hakikisha ndizi hazizami zote kwenye supu,bandika jikoni kwa moto wa kiasi  na ziache zichemke,geuza na kisha weka mafuta ya kupikia (na nazi tui la kwanza ukipenda) Acha ziive kabisa bila kuwa na kiini katikati ukiridhika kuwa zimeiva ipua.
Andaa meza tayari kwa kula ni chakula kitamu sana pembeni ukiwa na juice,chai au maji ya kunywa pamoja na matunda kama avocado  mlo unakuwa umekamilika



Maoni 2 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Adela hii tabia si nzuri kutamanisha watu hivi. Mwanadada mchokozi wewe:-) Yam yam yam ...

Unknown alisema ...

Nilipoona Nyama tu apetite ikaanza kudrop down.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom