Mahitaji ya pishi hili ni pamoja na ndizi mshale kiasi unachopenda kulingana na familia yako, nyama ya ng'ombe nusu kilo vitunguu maji vikubwa viwili nyanya moja pilipili hoho moja, karoti moja, mafuta ya kupikia kijiko kikubwa kimoja na chumvi kiasi..Jinsi ya ya kuandaa na na kupika anza kwa kuosha nyama vizuri na katakata vipande vidogo unavyopendelea na kisha chemsha hadi iive.Nyama yenye mafuta kidogo na mifupa kidogo inafaa sana kwa ndizi, kisha menya ndizi zako vizuri na kuzikata katikati kwa urefu na kisha kwa upana (msharazi) kisha zioshe na kuweka kwenye sufuria yenye maji masafi. |
Maoni 2 :
Adela hii tabia si nzuri kutamanisha watu hivi. Mwanadada mchokozi wewe:-) Yam yam yam ...
Nilipoona Nyama tu apetite ikaanza kudrop down.
Chapisha Maoni