Jumatatu, Aprili 11, 2011

Marehemu Elizabeth Taylor historia yake katika mahusiano ya kimapenzi na ndoa zake nane........

Marehemu Elizabeth Taylor pichani enzi za usichana wake atakumbukwa kutokana na umahiri wake wa kuigiza,lakini pia hawezi kusahaulika kutokana na ndoa zake nane ambazo kila moja ilikuwa na hadithi ya kuvutia
Aliolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1950 na tajiri wa mahoteli Conrad Nicky Hilton na ndoa hiyo ilidumu kwa muda wa miezi nane tu, kabla ya kifo chake Taylor aliwahi kusema kuwa ndoa hiyo ilidumu kwa wiki mbili ni baada ya kuonja machungu ya ndoa.

Mwaka 1952 aliolewa tena na mwigizaji Michael Wilding, huyu alifanikiwa kuzaa naye watoto wawili hata hivyo aliachana naye miaka minne baada ya ndoa

Miezi michache baada ya kuachana na Wilding alifunga ndoa na mwanamume ambaye kwa madai yake alikuwa ni mpenzi wa maisha yake Mike Tod kama wanavyoonekana enzi za uhai wao.Baada ya miezi 13 baada ya kufunga ndoa na Tod mume wake huyu alifariki dunia katika ajali ya ndege  nchini Mexico  wakati akiomboleza kifo cha Tod tayari alimgeukia rafiki yake kipenzi,

Baada ya muda alifunga ndoa na rafiki yake kipenzi Eddie Fisher kwa ajili ya kutuliza moyo wake na kupelekea jamaa kumuacha mke wake kwa ajili ya Elizabeth na hii ikiwa ni ndoa ya nne kwa mwanamama huyu,ndoa hii ilidumu kwa takribani miaka mitano.

Wakati akiigiza filamu  ya Cleopatra alikutana na mwigizaji Richard Burton na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi , lakini kipindi hicho alikuwa bado ameolewa na Fisher ,Baadaye uhusiano wao haukuwa siri tena wote wawili waliachana na wenza wao  na kuoana mach,15,1964 na kuachana miaka kumi baadaye lakini katika hali ya kushangaza walikuja kuoana tena mwaka 1975 na kudumu kwa muda.


Mwaka 1976, Elizabeth Taylor aliolewa na mwanasiasa John Warner ambaye aliachana naye mwaka 1982.

Michael Jackson na Taylor walikuwa marafiki na alimsaidia sana katika kukamilisha ndoa yake ya mwisho na Larry Fortensky, Michael alisimamia mpango mzima wa ndoa na ilifungwa nyumbani kwake mwaka 1991


Elizabeth Taylor na Mume wake wa mwisho Larry Fortensky ambaye pia aliachana naye baada ya miaka mitano na kusema kuwa asingeolewa tena. Kati ya waume hao saba aliowahi kufunga nao ndoa ni wawili tu walio hai, ambao ni John Warner na mume wake wa mwisho  Larry.


Marehemu Elizabeth Taylor amefariki  tarehe 23, March 2011 akiwa na umri wa miaka 79 kutokana na matatizo ya ugonjwa wa Moyo ameacha watoto ambao ni Michael Wilding,Christopher Wilding,Liza Todd na Maria Burton.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.




Maoni 2 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Astarehe kwa amani Mungu alitoa, Mungu ametwaa. Amina

Simon Kitururu alisema ...

Mwanamke wa SHOKa alikuwa huyu kwa kuwa alichokitaka alikitokea kichwa kichwa kuanzia wanaume mpaka mablingbling hasa ukifikiria jinsi watu waonavyo nisha kutokea wakitakacho!

NI mtazamo tu huu!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom