Jumamosi, Aprili 09, 2011

"Mwaka wa saba tangia mke wangu aniache lakini kanisa linakataa mimi kuoa mke mwingine"

Nimepata ujumbe huu kutoka kwa John labda mdau unaweza kumsaidia kwa ushauri,,"Mimi naitwa John nina matatizo mimi na mke wangu tulishatengana na kwa sasa imeshapita takribani miaka saba, nimechoka maisha ya kuishi mpweke natamani kuoa mke mwingine, sasa tatizo linakuja kanisa linakataa mkristu kuoa kwa mara ya pili na hawataki kuvunja ndoa yangu ya kwanza na mimi nataka kuanza maisha mapya kwa kuoa mwanamke ninayempenda sijui nifanyeje naombeni ushauri"

Maoni 2 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Mmmmh! kwanza pole sana, lakini wao hawajui ni shida gani ninyi mlikuwa naye. Je ninyii mwenyewe bado mnapendana au ni marafiki kiasi kwamba mnaweza kuongea na pia kuongea na wakubwa wa kanisa kuwa maisha yenu ya pamoja hayatakuwa mazuri tena? Na mnaomba ndoa yenu isiwe ndoa?

Bila jina alisema ...

Kaka cha kukushauri fuata moyo wako unataka nini kanisa au Askofu hakupeleki mbinguni ni wewe na Mungu wako cha msingi kama una watoto wachukue uwalee wewe.Makanisa yako mengi unaweza kufunga ndoa sio ilo tuu , sasa mtu anakukataza usioe na mke hukai nae yeye mchungaji yuko anakula raha zake na mke wake.
FANYA MAAMUZI YAKO NA UMSHIRIKISHE MUNGU MWANADAMU SI KITU.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom