Jumanne, Aprili 26, 2011

"Naomba ushauri nifanyeje ili nimuache mpenzi wangu wa zamani kwani naogopa kumwambia kuwa simtaki tena"

Dada Adela  mimi ninaomba ushauri  ishu yenyewe ni hivi.Mimi ni mvulana miaka kama mitatu nilikuwa na mahusiano ya kimapenzi na msichana mmoja jijini Mbeya kabla ya kuja Dar. ukweli ni kwamba msichana huyo ananipenda sana mpaka sasa ila mimi upendo nilionao simfikii yeye nikiwa na maana mimi sio kivile nilipokuwa nikifikili kwamba kwasababu sina upendo kama alionao yeye kuna binti mmoja alipita mbele ya macho yangu ukweli nilizima nilimfatilia sana hatimaye nikabahatika akawa kwenye himaya yangu sasa yule binti wa zamani bado ana upendo kama zamani na huyu wa sasa naye ndo usieme.Ukweli ni kwamba wote hawa wananipenda sana  kwa kuwa mimi sina tabia za kudungadunga sasa nifanye nini ili tuachane na huyu wa zamani na kumpa laivu naogopa ntamuumiza sana na pia huyu wa sasa hajui kama nilikuwa na m2 zamani.Plz naomba ushauri wako
                                                                    God bless you. 

Maoni 2 :

emuthree alisema ...

Hakuna kitu muhimu katika mahusiano kama kuambiana ukweli, ukweli unauma, lakini maumivu yake sio sawa na kudanganyana halafu mwenzako akaja kugunudua.
Kwa ushauri wangu, tafuta muda mwambie mwenzako ukwelii na hali ilivyo, na umsikie atasemaje, najua kama yeye ni mkweli akasikia huo ukweli atajua nini la kufanya...LAKINI, HEBU JIULIZE UNGEKUWA WEWE NII UPANDE WA HUYO MWENZAKO UNGEJISIKIAJE?

ADELA KAVISHE alisema ...

ushauri kutoka kwa wadau facebook,,

Saada Ali: Mwambie ukweli japo utamuumiza kwani kumficha kunaweza kumuumiza zaidi kuliko unavyofikiria sasa

Jerry Mussa Ng'onye: Kama mnamawacliano nae ctshaa..na kaanae mbal utamsahau taratbu...

Muntala Talavencha: Kwann uachane nae? Humpend? Amekukera ? Umemchoka? Hakufkish? Hakupend? Kwann ustafte suluh kujua nn tatizo? Me nadhan usmuache kama mlipendana wenyewe kwann tuwatenganishe? Nafs kwa nafs ..ila kisaikolojia ni kwamba umesema ufanye vp Ili uachane na MPENZ WAKO WA ZAMAN?ina mana kwa xaxa umepata mpya ama? Na mpaka wamuita wa zaman kwann?

Hamiar Mohamed: daa! na muonea huluma ok! mi nita kupa ushauli waku tosha endapo uta npa lizon kwa nn una mwacha hapo ndipo nta kusaidia huwez kujenga bila kuanza na msingi chazo nikp paka umwache mwezio

Saada Ali: uyu kaka ameeleza sababu vizuri Hamiar angalia katika blog ya Adela utaona msaidie kumshauri

Kwa mtazamo wangu naona unafanya jambo la hatari kuwa wapenzi wawili kwa wakati mmoja nivema akafanya maamuzi mwenyewe kuliko sisi maana yakikuadhiri kwa namna moja lawama zote zitakuwa juu yetu na urafiki utakufa. Kitu cha pili ni mpenzi w...See More

Mohamed Kombo:
Kama unaogopa bac u ctl lv da person so dnt bothr try'n 2 dump dat p yoh


Seleman Lyimo: anajua wewe ni mtamu mbaya zaidi ulimwonjesha asali sasa ametengeneza mzinga kazi ipo wangu pole sana cha kufanya kama aumfeel mwambie kuna kiwanja maali alafu angalia uwezo wake kama mdogo mwambie kinauzwa milion kadhaa kama tarakimu kubwa mwenyewe atamwaga manyanga


Edward Mwingira: bro Sele mapenz ukiingiza mali/fedha hayadumu.ushauri wako hapana aisee

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom