Jumatano, Aprili 27, 2011

Mapenzi ni matamu lakini usikubali yakuendeshe

Inapendeza kuona wapenzi wanapendana na kufurahi pamoja wakati wote lakini huwa inakuwa mbaya pale mmoja anapoonyesha kumpenda mwenzie zaidi na yule anayependwa akiwa hana mpango wa kujali mapenzi anayoonyeshwa,,hali kama hii uwakuta watu wengi ambapo unaweza kusema ni kupenda bila ya kujielewa kutokana na kushindwa kujiamini na kuogopa kulipoteza penzi la yule unayempenda, ni muhimu kujiamini kwa mwanadamu mbele ya mapenzi na usijishushe thamani hata kama umempenda mtu kupindukia, kupenda ni haki yako ya msingi lakini usiwe mtumwa wa mapenzi kwa kushindwa kujitambua wewe mwenyewe , fahamu kwamba kupenda ni kitu kizuri lakini ukizidisha inakuwa sumu inayokutafuna taratibu na yote ni kwasababu hujiamini na kujikuta ukiogopa kuachwa au kuachika na kuamini kwamba hakuna mpenzi mzuri kama uliyenaye na kuona kumpata kwako ni bahati na hivyo kujikuta hauna maamuzi yako binafsi lolote utakaloambiwa unakubali haijalishi ni zuri au baya

Ni lazima kuwa makini katika mapenzi  pia ni muhimu kutambua je unayempenda ana mapenzi ya dhati kwako ni wazi wapo wanawake kwa wanaume wakiteseka ndani ya mapenzi yao kwa penzi la upande mmoja, unalazimisha penzi kwa vile tu unampenda na kuona hakuna kiumbe chochote mbele yako usiwe kipofu wa mapenzi usihadaike na sura pesa angalia mapenzi ya kweli kwani matendo mema ndiyo yanayojenga upendo ndani ya nyumba,,usiwe mtu wa kuburuzwa kuwa na msimamo muhimu ni kuwa na mapenzi ya dhati heshima na upendo vitawale ndani ya nyumba.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom