Bi Aisha ambaye ni mfanyakazi wa saluni nilikuwa nikizungumza naye kero anazokutana nazo akiwa katika kazi yake akasema "kiukweli kero zipo ambapo mtu mwingine anaweza kuja anataka kusuka nywele ni chafu ukimuambia tuoshe kwanza anakataa na kingine ni baadhi ya wanawake kufika saluni na kuanza kuzungumza mambo yao ya ndani si tabia nzuri unakuta mtu anamsema mume wake mambo ambayo wanayafanya chumbani mwao maneno ya aibu na wakati huo hapo saluni wateja unakuta wapo wengi mimi hii tabia huwa siipendi na hata baadhi ya wafanyakazi wa saluni pia huwa wanakuwa na makosa kwani wakati mwingine akiwa anamtengeneza mteja ataanza kumuuliza maswali mengi mara umeolewa,,unaishi wapi na nani,,alimradi tu apate maneno na yule mteja akimsimulia si kwamba atabaki nayo yeye pekee bali wakija watu wengine ataanza kuwahadithia na ndipo baadaye unakuta watu wanasutana kwasababu ya umbea mimi ningependa kusema mwanamke kama umeenda saluni basi fuata kilichokupeleka tengeneza nywele zako na mambo mengine lakini siyo kuzungumzia maisha yako kwani si wote unaowasimulia ni watu wazuri kuna wengine hawapendi maendeleo ya watu ni watu wa kusikiliza na kusambaza maneno mwishowe wewe unabaki kuonekana mjinga tuwe makini jamani" alisema Aisha |
Maoni 3 :
Wanasema MWANAMKE KWA UMBEYA NI SAWA NA PILAU NA KACHUMBARI...Sijui, hayo sio yangu, bali nimeusikia huu usemi hapa jirani yangu!
Nimeshukuru sana leo kuona umenena kitu kijiweni kwangu..SHUKURANI NA KARIBU TENA!
adela pliz hiyo saluni iko wapi na je kuna contact ambayo twaweza tumia kumpata pliizzz nimependa hiyo yeboyebo
salma
mdau saluni ipo maeneo ya chang'ombe unaweza kuwasiliana na mimi nitakuelekeza 0652343430
Chapisha Maoni