Jumatatu, Mei 30, 2011

Jisikie huru kuwa na yule umependaye,,haipendezi kuwa na mapenzi ya siri

Inapendeza kuwa huru na yule umpendaye, haipendezi kuwa na mapenzi ya siri kwani kuna baadhi ya watu wana tabia hii unakuta mtu ana mpenzi wake lakini hapendi watu wajue kama wanamahusiano,  na hii tabia ipo kwa wanawake na wanaume,, hivi ni nini hasa kinapelekea tabia hii??? mimi naamini mtu unayempenda utakuwa naye huru wakati wote vinginevyo kama mapenzi hayo yatakuwa ya siri basi kuna tatizo..

Maoni 6 :

Bila jina alisema ...

WALIO WENGI WENYE TABIA HIYO WAHUNI MTAZAMO WANGU HUO LAKINI.

emu-three alisema ...

Raha ya mapenzi ni kujisikia na vyema ya kujisikia ni kuwa huru na mwenzako, au sio...ujumbe murua mpendwa. TUPO PAMOJA

Simon Kitururu alisema ...

Tatizo ni kwamba,...
....MAISHA hayana fomwula na mara nyingi MAISHANI matatizo hayakosi kuwepo.

Na kwa kuwa na MAPENZI nayo hayana FOMWULA ukichanganya na MAISHA kihali halisi watu hujikuta pia kuwa WAKO na MPENZI ambaye kawa ni MAZOEA TU au ambaye wameshajifunga naye KIUCHUMI wa FAMILIA, kiimani za DINI ambazo huweza kugeuza heshima ya MTU katika jamii kama akiachika au hata KIJAMII ukizingatia mapenzi ya watu wa WILI ki mila nyingine huunganisha KOO au hata MAKABILA mawili tofauti kitu ambacho ukimuacha aliyekuwa MPENZI wako MKE au MME inamaanisha unaporomoa mahusiano ya zaidi ya WATU wawili ,...
.... na hapa wala sigusii hata ya WATOTO ambao wanaweza kuwa ni matokeo ya wapenzi wawili ambao wako katika penzi lilokufa.

Nachojaribu kusema ni kuwa:
WATU wengi ambao wako mpaka kwenye ndoa ambazo ni za kimaigizo wakiwa nje ya NYUMBA ili watu wadhani wana amani na kupendana nje ya NYUMBA huku hata chumba ndani ya nyumba hawashei huwa HAWAJITAKII.

Watu huweza kujikuta wamefungwa na mambo mengine mbalimbali na kitokeacho ni kuwa na wapenzi wa siri.

Na kikubwa kifanyacho wengi wana wapenzi wa SIRI ni utumwa wa watu utokanao na kutaka ``KUJITUZIA HESHIMA ´´ na kwa hiyo kufanya mengine siri!


Na tukiachana na niliyosema hapo juu:
BIANDAMU tuko tofauti . Na kuna wanogewao na mambo kwa kuwa tu yanafanyika kwa siri.... na SIRI huwa ni moja ya UTAMU wenyewe. Na wengi wanogewao na mambo kwa siri. Kwa mfano yale ya kuonja mke wa mtu. Huwa huyo mke wa MTU akiachika huwa hawanogewi naye kisa yuko huru sasa kuonjwa kirahisi na usiri haupo tena. Na haya hutokea hata kwa WADADA wapendao WAUME wa watu ambao starehe ni kufanya nao kwa siri huku MDADA akijua kuwa baada ya MUDA lijamaa litarudi kwa mke wake na kumuacha huru bila bughudha... kitu ambacho kitaharibu utamu ikitokea kuwa ghafla huyuo kidume akaacha MKE na kusababisha awe na muda zaidi ambao huharibu utamu wa kuibia.

Ndio ,..
.... kuibia kwa wengine ndio UTAMU wenyewe.:-(

Kwa hiyo sentensi``...haipendezi kuwa na mapenzi ya SIRI´´ hapo juu kwenye kichwa cha habari,...
..... labda hutegemea tu MTU na MTU!:-(

Bila jina alisema ...

hongera sana Adela kwa blog yako nzuri tunapata mambo mazuri ni kweli kabisa mapenzi ya siri siyo ishu hata kidogo

Bila jina alisema ...

yaani mimi ilishanikuta mwenzenu mpenzi wangu alikuwa hapendi kutoka na mimi na alinikataza kabisa kuwaambia baadhi ya watu wake wa karibu juu ya uhusiano wetu baadaye nilikuja kugundua kumbe alikuwa na mchumba inauma sana

Bila jina alisema ...

Kwani unatangaza ni biashara hiyo?

Wakati kabla hamjakuwa na mahusiano mlitangaza wapi kutaka mahusiano hayo?mambo yenu ni yenu watu wengine mnaotaka kuwaambia yanawahusu nini kama siyo kukaribisha umbea?

Kwa nini watu hamridhiki na hali mlionayo na huyo umpendaye hadi utake akujulishe kila kona ya dunia? ndiyo maana hata mtu akiachwa huumia sana kwa sababu alijitangaza na kutangazwa huko na huko.

Tena muhimu ieleweke kabisa kuwa kuna mila na desturi zinatulinda sana hasa katika mahusiano ambayo ni nje ya ndoa huwezi kuwaambia watu kuwa huyu ni nani wangu lazima mjifiche hadi mtangaze ndoa muoane,lakini mambo ya mapenzi kwa mila zenu ni kama unajitangaza uhuni kwamba unahusika na mahusiano yasiyo halali.

Mnaofaidiana ni ninyi watu wawili,kwani mnataka kuwauzia maneno watu wasiowahusu?Ukitangazwa kuwa wewe ni nanihii wa fulani inakuongezea nini katika mahusiano hayo?

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom