Jumanne, Mei 17, 2011

katika mahusiano Mwanamke anaweza kuwa mzuri katika kila idara lakini akawa hajui kupika,

Mwanamke ni mama katika familia na kwa mwanamke yeyote aliyekamilika ni lazima ajue kupika, ni vizuri kujifunza kupitia vyanzo mbalimbali kama vitabu, mitandao nk angalau ujue namna ya kupika kwani ni aibu mwanmke umeolewa ndani ya nyumba haujui kumpikia chakula mume wako kila siku mnaenda kula hotelini na kibaya zaidi mwanamke wa namna hii unakuta hapendi hata kujifunza yeye anaona ni sawa tu na yote haya unakuta chanzo ni malezi namna alivyolelewa au mwingine atakuambia hana muda kutokana na majukumu, lakini kumbuka hata kama wewe muda mwingi upo bize lakini vizuri ukafahamu kupika vyakula mbalimbali angalau ukipata muda umpikie mumeo chakula kizuri na kitamu,

  Vilevile jifunze kupangilia vyakula siyo kila siku unapika wali nyama badilisha vyakula ili kuongeza mvuto na kuweka utofauti. inawezekana mwanamume kutafuta nyumba ndogo kwasababu tu mke wake hajui kupika na katika hili  hata mwanamume inabidi uwe wazi kwa mwenza wako kama unaona hajui kupika vile unavyopenda basi muelekeze mtafutie vitabu nk ili afahamu kupika na si kuchukua maamuzi ya kutoka nje ya ndoa. JAMANI WANAWAKE TUWE WABUNIFU TUJIFUNZE KUPIKA VYAKULA MBALIMBALI.

Maoni 4 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Wazo zuri ...nina swali je ni lazima mimi mwanamke tu nimpikie mume wangu? Je Mume wangu hawezi kunipikia mimi?..ni wazo tu ruksa kupinga...

Bila jina alisema ...

Hii theory yako inaappy kwa culture yetu tu ya Tanzania. Lakini culture zingine sio kweli na sio lazima mwanamke kujua kupika kabisa. Ni 50/50 kwa wengine na wengine wanaume ndio wapishi wakuu katika familia. Sasa hapa ni mwanamke atakakoolewa au kuishi ndio itakua jawabu. Mwanaume wa kibongo akioa mwanamke toka USA ajiandae kupika. Wanawake wao wasiopenda kupika wala hawasumbuliwi au kuulizwa kwanini. Sio jadi yao lazima mwanamke kujua kupika

Bila jina alisema ...

mwe asante dally mie nimeanza kujifunza kupika kupitia blog ya mapishinacecy.blogspot.com , ninajua kupika chapati , nilikua sijui kabisaa, hahaha, pitieni mtajionea

wiseman ficky alisema ...

Kupika ni lazima na sio hiyari,mke ni lazima ampikie mumewe ingawa pia cku moja moja mume anaweza kufanya hivyo.
Mfano hai mmeoana na mna watoto je itakuaje kila cku mkale hotel ikiwa kipato chenu hakiruhusu. Ni aibu kwakwel mke kushindwa kumpikia mumewe!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom