Jumatano, Mei 04, 2011

"kuwa na malengo kwanza ili kupata mafanikio"

Mtangazaji wa kipindi cha taarabu AMBAA NA MWAMBAO  radio Passion fm Warda Chande leo katika kipindi chake nimeupenda ujumbe huu  "katika maisha ni muhimu kuwa na malengo ili uweze kufanikiwa huwezi kukurupuka kufanya jambo fulani bila kuwa na malengo nacho,, kwa mfano unataka kufanya biashara yoyote ile hata kama unaanza na mtaji mdogo ni vizuri kujipanga na kuwa na malengo kwa kile unachokifanya ili upate mafanikio, amewazungumzia wanawake zaidi akisema

"wanawake baadhi wamejibweteka sababu ikiwa  ni kutegemea pesa za wanaume kutokana na kwamba kila anachokihitaji anakipata basi haangaiki kufikiria kufanya shughuli yoyote ile na mwisho wake anabaki kuwa tegemezi maisha yake yote hawezi kusimama yeye kama yeye, na pia unaweza kukuta mtu anauwezo lakini hana malengo na hajui nini afanye ni muhimu kuomba ushauri na kusikiliza ushauri unaopewa kwa manufaa yako,, akamalizia kwa kusema tuwe na malengo ili tuweze kufanikiwa usisubiri mtu mwingine akuwekee malengo jitambue na simama imara kila kitu kinawezekana kwa juhudi na malengo

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom