Ijumaa, Aprili 29, 2011

Ujumbe wa weekend "sikiliza maneno ya watu na ufanye uchunguzi" kwani yawezekana lisemwalo lipo"

Katika maisha tunakutana na mambo mengi sana yakiwemo mazuri au mabaya yawezekana ikawa ni katika mapenzi au katika maisha ya kawaida katika kazi zetu nakadhalika na tunakutana na watu tofauti na kila binadamu ana tabia yake,, unaweza kuwa na rafiki ambaye anakupenda na akawa anakupa maneno yanayomuhusu mtu wako wa karibu inawezekana yakawa yanamuhusu mpenzi wako au rafiki yako  maneno haya usiyapuuzie na wala usiyachukulie hatua yoyote kwa wakati huo jaribu kumskiliza na baada ya hapo fanyia uchunguzi ili uweze kupata ukweli kamili kwani wengine huwa wanakurupuka na baadaye wanajuta kwa nini nilisikiliza maneno ya watu na kuchukua uamuzi wa ghafla,,na tukumbuke majuto ni mjukuu ni vyema kutafakari mapema kabla haujachelewa maneno ya watu yanaweza kuleta migogoro katika familia, mapenzi ,kazini, na marafiki kugombana ni muhimu kuwa makini Weekend njema wadau

Maoni 3 :

Unknown alisema ...

Umegusa na kuwazisha.

Changamoto ni nyingi kila inapoitwa siku.

Simon Kitururu alisema ...

Asante kwa Shule!

emu-three alisema ...

Na kweli ndugu yangu ujumbe murua, lisemwalo lipo kama halipo laja!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom