Jumatatu, Mei 23, 2011

Ni muhimu kuweka akiba kila unapopata fedha bila kujali ni kiasi gani ulichonacho.

Ni muhimu kujijengea tabia ya kuweka akiba kwani ni wazi kabisa baadhi ya watu tabia hii ya kujiwekea akiba kwao wanaona ni jambo gumu sana, lakini kumbuka tabia ya kuweka akiba ni kwa manufaa yako na  inakuwezesha kuwa na nidhamu nzuri ya matumizi ya fedha zako na pia itakusaidia kukuinua kiuchumi, lakini tabia ya kuweka akiba ni hali ya mtu kujitoa na kumaanisha kwa kile anachokifanya bila ya kujali anapata kipato kiasi gani, na ni vizuri kuweka akiba pale tu unapopata fedha kamwe usisubiri kufanya manunuzi yako yote kisha iliyobaki ndiyo uweke akiba.

  Unatakiwa utoe kiasi unachoweka baada ya hapo ndiyo utumie kwa matumizi mengine, na kingine unaweza kukuta mtu anauwezo mzuri kifedha lakini anasahau kujiwekea akiba akifikiri kuwa pesa haziishi jamani kumbuka kuna leo na kesho hivyo ni muhimu kuweka akiba mapema na kama una familia ni vizuri hata Watoto wako au watu wako unaokaa nao ukawafundisha na kuwaelekeza umuhimu wa kujiwekea akiba ili kuwajengea msingi mzuri katika maisha


Naamini kwa sasa watu wengi wanaweka akiba katika Bank mbalimbali lakini pia wapo wanaohifadhi nyumbani  yote ni sawa ila ni muhimu kuwa na nia kwani bila nia unaweza kujikuta unatumia zile pesa ulizoziweka mara kwa mara, na kumbuka unapokuwa umejiwekea akiba hata likitokea jambo la dharula hautatetereka kwasababu utakuwa na kitu cha kuanzia hata kama ni kwa kiasi kidogo. AKIBA HAIOZI, TUKUMBUKE KUWEKA AKIBA WAKATI WOTE. KWA MANUFAA YETU .
n

Maoni 2 :

Rik Kilasi alisema ...

Kuweka akiba muhimu Adela umesema kitu cha msingi vijana wengi tukishapata fedha cha kwanza tuna fikiria zaidi starehe mwisho wa siku hata mshahara mwisho wa mwezi huuoni au mshahara wa mwezi uliopita hauungi ule unaokuja.Mwenye macho haambiwi ona wewe umemaliza kazi yako big up sana

Bila jina alisema ...

ni kweli kabisa kuna umuhimu wa kuweka akiba mara kwa mara inasaidia sana

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom