Jumatano, Mei 25, 2011

Je katika mahusiano kuna umuhimu wa kufahamu mali zote anazomiliki mwenza wako.??

Tazama picha hii halafu tafakari je ni kweli  kufahamu mali  anazomiliki mwenza wako ni kipimo cha mapenzi ya kweli? Katika mahusiano hususani kwa walio kwenye ndoa ni jambo la kawaida kwa mwanamke au  mwanamume kufahamu mali anazomiliki mwenza wake ikiwa ni pamoja na kazi anayofanya kiwango cha mshahara anachopata, magari kama anayo, nyumba na biashara nyingine anazofanya mbali na kazi yake, lakini pia katika hali hii wapo baadhi ya watu wasiopenda wenza wao wafahamu mali wanazomiliki.

katika upande mwingine kuna baadhi ya watu wanaotaka kufahamu nini anachomiliki mwenza wake kwa nia ya kuzipata hizo mali ziwe zake na hali hii hutokea hata kwa baadhi ya watu ambao hawapo kwenye ndoa utakuta mwanamke anataka kujua mali anazomiliki mwenza wake na mwanamume akisita kumuambia basi anaanza  kulalamika na kuona kuwa hapendwi  kitu ambacho kinampelekea yule mwanamume kuhisi huyu mwanamke amenipenda mimi au anapenda mali zangu? 

Jamani mimi naona kwa walio kwenye ndoa ni vizuri kuwa muwazi ili muweze kushirikiana katika kujiendeleza kiuchumi na kwa wale walio katika mahusiano kuwa makini usiwe na haraka ya kutaka kufahamu kila kitu anachomiliki mwenza wako kiukweli anaweza kupata mawazo tofauti na kufikiri kuwa unapenda mali zake. MUHIMU NI KUWA MAKINI KWANI WAPO WALIO KATIKA MAPENZI KWASABABU YA PESA NA WAPO WALIO NA MAPENZI YA KWELI

Maoni 2 :

Hashir alisema ...

Ade,
Upo sawa kabisa, katika mahusiano ya kindoa, mtu unahaki zote za kutaka kujuwa mali anazomiliki mwenziwe, na pia kama unamiliki mali fulani, basi unawajibu kumueleza mwenzio umiliki wako ni upi na upi. Lakini pia, inafaa kumueleza mwenzio kama unadaiwa wapi na wapi, ili nayeye afahamu katika mali zako, basi kuna deni unalodaiwa na mtu fulani au kampuni fulani.
Kuhusu wale wasiokuwa katika ndoa, nikweli kabisa, haifai kuuliza kila wakati, ukitaka kujua mpenzi wako anamiliki nini na nini, coz sasa dunia imeharibika sana, mtu utamuona anakupenda saaaana, kumbe anajuwa unamiliki nini na nini ili aendelee na mapenzi ya ulaghai, ila kunawakati mwengine, mapenzi ya kweli yanajionyesha wenyewe, na unakuwa radhi kumueleza mwenzio nini na nini unamiliki ili nayeye ajuwe!!, sasa hapa natoa tahadhari, kwawale wapenda sifa kwa wapenzi wao, usipate mwanamke au mwanaume leo ukaona anakupenda saana, basi ukaanza kumueleza kila kitu unachomiliki,ili akupende zaidi, hapo utakuwa unajichimbia shimo, nibora mukachunguzana kwanza kabla ya kuambizana ya undani!!..

emu-three alisema ...

Mapenzi sio mali, ni hisia. Mkipendana kwa dhati mambo mengine yatajileta tu!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom