Ni wazi kabisa wawili wanapopendana na kuwa pamoja kuna baadhi ya watu huwa na chuki binafsi chanzo ikiwa ni wivu, ambapo inawezekana anapoona mwenzake yupo katika mahusiano na mtu ambaye anampenda, anamjali na muda wote wapo katika furaha na huku akiangalia kwa upande wake mahusiano aliyonayo hakuna amani basi akiona mwenzake mahusiano yake yapo vizuri anachukia na kuwaza afanye nini ili aweze kuvuruga uhusiano huo na hapo ndipo ataanza kutafuta maneno ya uongo na kukuletea alimradi tu awakorofishe usipokuwa makini utajikuta unakuwa katika migogoro.
Muhimu kuchunguza kile unachoambiwa, kwani siyo wote wanapenda kukuona ukiwa na furaha.Kitu kingine ni kwamba kwa wale wenye tabia ya kuwa na chuki binafsi haipendezi kumfanyia mwenzio vibaya ni vizuri kutamani na kuwa na malengo ya kuitafuta furaha kama aliyonayo mwenzio kuliko kuchukia na kutaka kumuharibia kwani kwa kufanya hivyo haikusaidii chochote. Jamani tuwe makini kwani ni vigumu kumtambua adui yako inawezekana akawa ndugu yako,rafiki yako au jirani yako ...... |
|
Maoni 2 :
Lisemwalo lipo Adela, Kama halipo laja. Wapo wazushi ndio lakini hawazushi tu hivi hivi.
Kweli hiyo imo, wakati umepata kuna ambao hawajapata bahati hiyo, wanaombea lini wataipata, sasa ndiyo hiyo wengine wanakwenda rafu kuwatakia mabaya ili muachane wapate wao...au sio
Chapisha Maoni