Jumanne, Juni 14, 2011

Inawezekana rafiki yako wa karibu kuwa mpenzi wako.

Katika mahusiano inawezekana unaye rafiki ikiwa ni shuleni, kazini nk. kuna mambo yanayopelelekea baadhi ya marafiki kuwa wapenzi yaani zaidi ya urafiki kama ukaribu walionao hivyo kila mmoja kumfahamu mwenzie, na mambo mengine ambayo yanaweza kuwashawishi kuwa wapenzi bila kutarajia jambo la muhimu ni kuwa makini kwani inawezekana tayari unaye mchumba au upo kwenye ndoa lakini kwa wakati huohuo ukajikuta umeingia katika mahusiano na rafiki yako kipenzi na hali hii inaweza kuwa ni tamaa za mwanzo tu lakini baadaye ukajuta bora tungebaki kuwa marafiki lakini unakuwa umechelewa. KUWA MAKINI KATIKA HILI KWANI INAWEZEKANA

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

jamani Adela uko sahihi kabisa haya mambo yapo hata mimi ilikwisha nitokea

emu-three alisema ...

Duuh, ! Ndio maana mshairi mmoja akasema;

Fisi nyama atamani, hata kama kasinzia,
Pua yake ni makini, yahisi hata pazia
Unawaweka zizini, eti tunaishi nasi
Waona wapi jamani, mbuzi kulala na fisi.

Binadamu tulivyo tumeumbwa roho kutamani, mnaweza kupendana kwasababu ya ukucha tu...kwahiyo mkikaa pamoja kwa muda kuna kitu kitawavuta, kama si sauti, kama si sura, basi hata ukucha...ambapo labda mume anacho au mkeo anacho, ila tofauti ni ndogo tu, kitawavuta kujikuta mkijjiona kuwa mnapendana,lakini huenda sio kweli, ni sababu ndogo ya `hisia' ...
ni bora tu mkaweka mpaka kuwa `wewe ni rafiki yangu..wewe ni ndugu yangu...tusivuke hapa...
je yawezekana kweli, fisi na mbuzi wakakaa zizi moja, eti dada Adela?
TUPO PAMOJA DAIMA!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom