MaishaMema Education & Training Centre ni kituo cha utoaji Elimu, Mafunzo, Utafiti na Ukuzaji Maarifa...Kituo kinaratibu mradi wa elimu ya ujinsia kwa njia ya vitabu kwa wanawake/wasichana waliopo mashuleni, vyuoni, magerezani na maofisini " SEXUALITY EDUCATION & AWARENESS PROJECT " mradi ambao umeanza rasmi tarehe 1 JUNE 2011 kwa kuwashirikisha waandishi kumi na tano ( 15 ) kutoka katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam, na kwingineko.
Kituo kinatoa mkopo ( udhamini ) kwa waandishi wa vitabu wenye sifa zifuatazo:
1.Jinsia ya kike.
2.Umri miaka 18 hadi 45.
3. Elimu kidato cha nne, sita na kuendelea.
4.Awe na uwezo mkubwa wa kuandika kitabu ambacho kimefanyiwa utafiti wa kina juu ya masuala yanayo husiana na ujinsia miongoni mwa wanawake.( Kitabu chaweza kuwa cha kiingereza au kiswahili ).....
Tutatoa mkopo ( UDHAMINI ) juu ya gharama za uchapishaji wa kitabu pia Tutakipeleka kitabu Sokoni..Baada ya kitabu kuingia sokoni, Tutarejesha gharama zetu za mkopo pamoja na riba, kiasi cha pesa kitakacho baki kitakuwa ni mali ya mwandishi.
Fomu za maombi ya mkopo zinapatikana katika ofisi zetu zilizopo katika shule ya sekondari PERFECT VISION kwa shilingi Elfu Kumi na Tano Tu. ( Tshs.15,000/=).
Mwisho wa kutoa fomu za maombi ya mkopo ni tarehe 17/06/2011.
KWA MAELEZO ZAIDI, WASILIANA NASI KWA SIMU NAMBA: 0652458398 AU 0788363058
Au tembelea tovuti yetu : http://www.maishamematanzania.blogspot.com//
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni