Jumanne, Juni 14, 2011

Mume wangu hawapendi ndugu zangu inaniuma sana...........

Habari yako Adela mimi naitwa Salima ni mkazi wa Dar es salaam nimeolewa na katika ndoa yangu nina watoto watatu, maisha yangu na familia yangu ni mazuri lakini tatizo linakuja kwa mume wangu hawapendi ndugu zangu na mimi hao ndugu zangu nilikuwa nikiwasaidia kabla hata sijaolewa kwasababu mimi nafanya kazi na wazazi wangu hawana uwezo mkubwa, walinisomesha ili angalau baadaye nije kuwasaidia wadogo zangu.

Tatizo ni kwamba kila ninapowasaidia huwa namshirikisha mume wangu na sasa imefikia hatua mume wangu hatoi pesa za matumizi nyumbani anasema nitumie pesa ninazowapa ndugu zangu na pia ndugu zangu wakija kunisalimia pale nyumbani anaonyesha kukasirika na wakati mwingine wakimsalimia haitiki naumia sana kwani sasa inafikia hatua ananiambia nimchague yeye au ndugu zangu na mimi familia yangu wadogo zangu nawasomesha siwezi kuwaacha wateseke sijui nifanyeje.

Maoni 5 :

Bila jina alisema ...

pole sana Salima mimi nakushari ukae na huyo mumeo umueleze ni kwa kiasi gani ni muhimu kwako kuwasaidia ndugu zako vinginevyo huyo mwanamume hakupendi

Bila jina alisema ...

jamani mtu ukipenda boga penda na maua yake huyo mwanamume ana balaa kweli lazima atakuwa ni mbinafsi kama wewe unafanya kazi halafu hataki uwasaidie ndugu zako atakuwa hana utu kuwa naye makini

Bila jina alisema ...

naitwa John aunt mimi nakushauri ukae naye ili akueleze kwanini anawachukia labda kuna sababu.

Bila jina alisema ...

Ningependa kujua vp kwa upande wa ndg zake. Pia mwambie umuhimu wake kwako na umuhimu wa ndg zako kwako kwani hukushushwa kama mvua.

Bila jina alisema ...

Wewe endelea tu kuwasaidia ndugu zako maana usipowasaidia sasa kielimu utachonga mzigo mkubwa zaidi.Ikiwezekana achana na kumshirikisha mumeo juu ya misaada unayotaka kuwapa ndugu zako.Fanya siri.Kama ameacha hata kutoa matumizi home basi muombe Mungu sana akuwezeshe kupata nguvu kutunza ndugu zako kielimu.Ujue kuwa hao ndugu zako ndiyo watakaokutunza wewe ukilemewa hapo baadaye.Huyo mumeo kimeo kabisa na wako watu wa aina hiyo wala usikate tamaa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom