Kuna njia nyingi za kupata marafiki hii inategemeana na mazingira na maeneo, hata na hivyo rafiki si lazima awe ni mtu unayeishi naye karibu,kusoma naye,kufanya kazi pamoja kama biashara au kushirikiana katika mambo mbalimbali, unaweza kujenga mtandao mkubwa wa marafiki huku wengine usipate hata bahati ya kuwaona bali mkawasiliana kupitia mitandao kama faceboo,twitter,simu nk.lakini kumbuka kuwa makini kwani binadamu tunatofautiana kwani wapo walio na nia nzuri na wengine wanaweza kujifanya ni marafiki kumbe wana nia ya kukuangamiza yaani wanakuwa marafiki adui.TUDUMISHE URAFIKI NA UPENDO WAKATI WOTE BILA KUBAGUANA. |
Maoni 5 :
Hilo nalo neno my dear Adela big up sana ni kweli ni bora kuwa na marafiki ila tatizo wengi huja na nyuso za urafiki lakini kumbe wanafki wanakera sana
marafiki adui ni wengi sana ndugu yangu,,ni kweli tuwe na urafiki wa kushirikiana na kutafuta maendeleo na si wa kinafki uliojaa wivu na choyo ndani yake
Ni kweli , kwani urafiki wa kweli hukimbiza maadui
Ni kweli.
yaani hata ndugu yako anaweza kuwa adai yako mkubwa
Chapisha Maoni